Serikali nchini Kenya imesema kuanzia December 21,2021 Watu watalazimika kuonesha cheti cha kuchanjwa chanjo ya Covid 19 ili kuweza kupata huduma kwenye Ofisi za Serikali , wale ambao hawajachanjwa hawatopewa huduma.

Baadhi ya ofisi ambazo bila cheti cha chanjo Mtu hatopata huduma ni Mamlaka ya Mapato (KRA), Uhamiaji. Hospitalu, Shuleni na Vyuoni , Bandarini n.k

Waziri wa Afya wa Kenya Mutahi Kagwe amesema kuelekea kuanza kwa utaratibu huo kuanzia November 26,2021 kutakuwa na ugawaji chanjo kwenye maeneo yenye mikusanyiko ya Watu wengi kwa siku 10 mfululizo.

"Hakuna aliyesema chanjo ni lazima lakini kama unahitaji huduma kwenye Ofisi za Serikali unapaswa kuchanja"