Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametia saini Muswada wa Sheria ambao utazuia Wanawake ambao hawakuwa ndani ya ndoa yaani Michepuko (Mipango ya Kando) kutopata mirathi kutoka kwa Wapenzi wao pale wanapofariki.

Sheria hiyo inawataja wanaopaswa kupewa mirathi kuwa Mke rasmi anayetambulika, Watoto na wengine ambao wametajwa kwenye Sheria.

Lengo la Sheria hiyo ni kuzuia migogoro ya mara kwa mara inayotokea pale Mtu anapofariki ambapo wakati mwingine Wanawake zaidi ya watano wote hupambania mirathi.