Rais Samia Suluhu Hassan atakuwa mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani Desemba Mosi, 2021 mkoani Mbeya.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Novemba 22, 2021 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amesema Raisi Samia atahitimisha kilele cha maadhimisho hayo.

Amesema Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Akson atafungua maadhimisho ya kuelekea siku ya Ukimwi duniani Novemba 24 yatakayofanyika katika viwanja vya Ruanda Nzovwe jijini Mbeya

“Pia kuanzia Novemba 26-27 kutakuwa na kongamano la vijana ambapo tunatarajia atakuwepo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera, Ajira, Kazi, Vijana na Walemavu, Jenista Mhagama” amesema Homera.