Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametangaza vita na Magaidi wote nchini humo ambapo amewataka  wajisalimishe wenyewe ili waokoe maisha yao lasivyo wote watauawa.

"Tumewakamata washukiwa wa ugaidi 106 hadi sasa ambao wana uhusiano na matukio mawili ya milipuko ya hivi karibuni, bado tunawasaka wengine akiwemo Obaida Bin Bukenya. Ushauri wangu kwa magaidi wote wajisalimishe ili waokoe maisha yao, wasipojisalimisha wote watapoteza maisha

"Tunaongea na Serikali ya DR Congo tutawapata waasi wa ADF ambao wanashirikikiana na IS kuendesha ugaidi , Marais wa Nchi zote Afrika wamenipigia na tutalitatua hili tatizo la ugaidi

"Nawaomba watu wawe na subira wakati uchunguzi wa matukio mawili ya mlipuko ukiendelea, subirini watuhumiwa wafikishwe mahakamani mtasikia ukweli, Mimi ni msomaji mzuri wa masuala ya kijasusi, subirini Mahakamani" amesema Rais Museveni