China imeongeza kasi ya kutengeneza silaha zake za nyuklia kuliko ilivyotarajiwa, kulingana na makadirio ya vikosi vya jeshi la Marekani.
Ripoti ya kila mwaka ya wizara ya ulinzi ya Marekani iliyowasilishwa bungeni imesema kwamba China inaazimia kumiliki mabomu 1,000 ya nyuklia ifikapo mwaka 2030.
Wizara ya Pentagon imesema ongezeko hilo linawatia wasiwasi. Kuna uwezekano mkubwa wa China kuchukua nafasi ya Marekani kama taifa lenye nguvu zaidi ulimwenguni katikati ya karne hii.
Aidha kuongezeka kwa nguvu ya China kunahatarisha usalama wa Taiwan ambayo mzozo wake na taifa hilo umekuwa ukizidi kutokota hivi karibuni.