Tume ya Utumishi wa Mahakama ni chombo kilichoundwa kwa mujibu wa aya ya 112(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Aidha, Sheria ya Uendeshaji wa Mahakama Na. 4/2011 inaipa Tume ya Utumishi wa Mahakama jukumu la kuajiri watumishi wa kada mbalimbali
wa Mahakama pamoja na majukumu yake mengine.
wa Mahakama pamoja na majukumu yake mengine.
Hivyo, Tume ya Utumishi wa Mahakama inawatangazia Watanzania wenye sifa zilizoainishwa hapa chini kwa kila nafasi ya kazi na ambao wako tayari kufanya kazi katika Mahakama ya Tanzania katika Mikoa mbalimbali kuleta maombi yao ya kazi.
Nafasi hizo ni Hakimu Mkazi Daraja la II – (Nafasi 10) , Msaidizi wa Hesabu (Nafasi 3), Mhandisi wa Majengo (Civil Engineer) Daraja la II (Nafasi 1), Mhandisi Mkadiriaji Ujenzi (Quantity Surveyor) Daraja la II (Nafasi 1), Afisa Utumishi II (Nafasi 1) na Katibu Mahsusi Daraja III (Nafasi 4)
==>>Kujua Zaidi Pamoja na kutuma Maombi,BOFYA HAPA kupakua PDF