Fredy Kipara (38) ambaye ni
Shahidi wa tano upande wa Jamhuri katika kesi ya uhujumu uchumi yenye mashtaka ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake, ametoa taarifa za miamala ya fedha aliyoifanya Mbowe kwa nyakati tofauti.
Kwa mujibu wa Kipara, Mbowe alifanya miamaka mbalimbali kutoka kwenye simu yake ya tigo kwenda kwa mtu mwingine kiasi cha Sh.500,000.

Kapara ambaye ni mwanasheria wa Kampuni ya mtandao wa simu ya Tigo, aliyeajiriwa mwaka 2012 kitengo cha sheria, ametoa ushahidi wake jana  Jumanne, tarehe 2 Novemba 2021, katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Dar es Salaam.

Ametoa ushahidi huo akiongozwa na Wakili wa Serikali, Nasorro Katuga ambaye amemuuliza majukumu yake ya kila siku ni yapi na kujibu ni, kushauri viongozi maswala yanayohusu sheria, kutengeneza, kusoma, kupitia na kusaini mikataba.

Pia amesema kufuatilia, kusimamia kesi zote zinazohusiana na tigo kumsaidia vyombo vya ulinzi na usalama katika kupata taarifa mbalimbali kutoka kwa wateja zinapohitajika.

Kipara amesema, miongoni mwa vyombo vya usalama wanavyovisaidia kupata taarifa baada ya kuziomba kwa njia rasmi ya maandishi ni Polisi, Jeshi, Anga kama ni Ardhi na vyombo vyote vinavyofanya uchunguzi wa kisayansi.

Amedai taarifa zozote ambazo zitakuwa zinahitajika wao wanazo, kuna kupiga na kupokea simu za wateja wetu zinaitwa Call Details, taarifa za miamala ya fedha na kutuma na kupokea fedha

Pia, kuna Recharge ya vocha na kutumia pamoja na matumizi yake, taarifa za usajili na taarifa nyingine zote zinazoambatana kama Nida, locations na bill mbalimbali anazolipa.

Alipoulizwa hizo taarifa anazitoa wapi, shahidi amesema taarifa zote za kampuni pamoja na wateja wake zinakuwa stored kwenye Server ambayo inakuwa na ulinzi ili isiingiliwe na wana mitandao.

Mbali na Mbowe kwenye kesi hiyo wengine ni, Adam Kasekwa, Mohamed Abdillah Ling’wenya na Halfan Hassan Bwire, waliokuwa makomandoo wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ). Kwa pamoja wanatuhumiwa kupanga vitendo vya kigaidi.

Mahojiano baina ya mwanasheria wa Tigo na wakili wa serikali yalikuwa hivi;

Shahidi: Tigo- taarifa zote zinakuwa Served Automatically mtu anapo piga simu mnara unasoma na taarifa zinashuka na zina switch na kwenda Automatically kwenda kwenye server kuwa stored

Wakili wa Serikali: Ishu ya kuvisaidia vyombo vya Ulinzi na usalama utaratibu ukoje

Shahidi: Kila chombo cha ulinzi kinahitaji kuwa na hizo document iwe amri au ombi lazima iwe In writing

Wakili wa Serikali: In Writing unamaanisha nini

Shahidi: Iwe na Proper heading, Iwe na Nini wanataka

Wakili wa Serikali: Kwa hiyo ni barua lazima iwe hivyo

Shahidi: Ni barua au order ya Mahakama

Wakili wa Serikali: Kwa kumbukumbu zako Mnamo tarehe 02 Julai 2021 ulikuwa wapi

Shahidi: Nilipata barua mbalimbali za maombi, katika barua hizo kuna barua ilitoka  kwa kamishina wa upelelezi wa kisayansi ikihitaji taarifa za namba ya mteja

Wakili wa Serikali: Ulisema kuna aina mbili za maombi kuwa kuna maombi na amri Je, hiyo ilikuwa nini

Shahidi: Ilikuwa ni Requeast

Wakili wa Serikali: Unaweza kukumbuka ilikuja kwa maombi ya kuomba taarifa fulani za namba fulani Je, unaweza kukumbuka? Hiyo namba uliyoombewa kwenye Hiyo barua

Shahidi: Baada ya kuifikiria anaitaja 0719933386

Wakili wa Serikali: Hilo ombi lilikuwa ni maombi mangapi

Shahidi: Yalikuwa maombi ya miamala ya fedha na usajili.

Wakili wa Serikali: Baada ya kupokea sasa, nini ulifanya kuhusiana na ombi hilo

Shahidi: Nilipopokea ombi kutoka kwa kamishina, niliingia kwenye kompyuta yangu, nikaweka Credentials zangu, nikafunga screen server, nikaingiza namba ya simu kwenye procedure ambayo inaniruhusu kupata Tigo Pesa

Wakili wa Serikali: Unakumbuka ilikuwa ni yawakati gani

Shahidi: Walitaka taarifa za miamala ya fedha kutoka 01 June ya 2020 mpaka 31 June ya 2020. Nikaingia kwenye kompyuta nikaziona na kuzi print kisha nikaingia namba kuona taarifa za usajili.

Wakili wa Serikali: Kwenye namba uliyotaja baada ya kuprint ukafanya nini

Shahidi: Niliandika barua kumjibu kamishina wa makosa ya kisayansi alichokuwa anakitafuta nikamrudishia. Katika barua nilisha print lazima nigonge muhuri na signature yangu na lazima muhuri wa MIC Tanzania Ltd

Wakili wa Serikali: Ukiambatanisha na nini hiyo barua

Shahidi: Cover letter, barua ya kamishina, miamala ya kifedha na usajili.

Wakili wa Serikali: Shahidi tufafanulie Maneno kama sender maana yake nini

Shahidi: Send My Op namba 0719933386 Receiver 0787555200, Muamala wa tarehe 20 Julai 2020 Sh.500,0000 saa 2:21 na salio ilikuwa Sh. 2.3 milioni

Wakili wa Serikali: Twende kwenye hii ya usajili

Shahidi: Imeanza na namba pale juu. Jina la kwanza jina la katika, Taifa, jenda na vitu vinginevyo. Mstari unaofuata 0719933386 Jina Freeman Last name Mbowe

Wakili wa Serikali: Tarehe 20 Julai 2020 inaonekana nini

Shahidi: Kuna namba ya Tigo ya 0719933386 imetuma kiasi cha fedha laki tano kwenda kwa namba ya Airtel namba 0787555200

Credit: Mwanahalisi