Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini Kenya (DCI), George Kinoti amehukumiwa kifungo cha miezi minne jela kwa kukaidi agizo la mahakama ililomtaka kurudisha bunduki za mfanyabiashara.

 Kinoti ametakiwa kujisalimisha ndani ya siku saba na iwapo atakaidi agio hilo, Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ameagizwa kutoa hati ya kumkamata.

Mwanzoni mwa mwezi Januari mwaka huu, Kinoti alipewa siku 30 na Mahakama Kuu nchini humo kuhakikisha anarudisha bunduki na risasi zote zilizochukuliwa kutoka kwa mfanyabiashara, Jimi Wanjigi lilitolewa kama ilivyoagizwa mwaka 2019