Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawafahamisha wateja wake kuwa, Jumatatu Novemba 15, 2021 kutakuwa na matengenezo ya njia ya kusafirisha umeme wa kilovolti 220 kutoka Kidatu hadi Iringa kuanzia saa 12:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni.

SABABU:

Kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme katika gridi ya Taifa.

Kutokana na matengenezo hayo kutakuwa na upungufu wa umeme kwa baadhi ya maeneo ya mikoa ya Mbeya, Njombe, Ruvuma, Singida, Shinyanga, Mwanza, Mara, Tabora, Arusha, Kilimanjaro na Tanga.

Tunawaomba radhi watejawetu kwa usumbufu utakaojitokeza.

Tafadhali usishike wala kukanyaga waya uliokatika, toa taarifa dawati la dharura la wilaya kwa msaada zaidi au Kituo cha Miito ya Simu Makao Makuu:+255 222 194 400 na +255 768 985 100