Marekani imemaliza vikwazo vilivyowekwa dhidi ya Burundi miaka sita iliyopita, ikitoa mfano wa mageuzi nchini humo.

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilibainisha kuwa Rais Joe Biden alibatilisha amri iliyoidhinisha vikwazo hivyo.

Ilikubali uchaguzi wa mwaka jana ambao ulimleta Rais Évariste Ndayishimiye na mageuzi ambayo amefuata "katika sekta nyingi".

"Tunatambua hatua zilizoafikiwa na Rais Ndayishimiye katika kushughulikia biashara haramu ya binadamu, mageuzi ya kiuchumi, na kupambana na rushwa na kuhimiza maendeleo endelevu," Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alisema.

Naibu Katibu wa Hazina ya Marekani, Wally Adeyemo, alisema katika taarifa tofauti kwamba Marekani itaendelea kuishinikiza Burundi "kuboresha hali ya haki za binadamu nchini humo na kuwawajibisha wale wanaohusika na ukiukaji na unyanyasaji".

Marekani na Umoja wa Mataifa ziliweka vikwazo dhidi ya Burundi mwaka 2015 - ikiwa ni pamoja na vikwazo vya visa na kufungia mali za maafisa wakuu serikalini.

Ilikuja baada ya nchi kuingia katika machafuko baada ya Rais Pierre Nkurunziza kuzindua azma ya kuwania muhula wa tatu madarakani

 

Credit:BBC