1.0 UTANGULIZI

1.                 Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba, Bunge lako Tukufu likaekama Kamati ya Mipango ili kupokea na kujadili mapendekezo ya Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka 2022/23.


2.                 Mheshimiwa Spika, awali ya yote napendakutumia fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuendelea kutujalia uhai na afya njema na kutuwezesha kukutana ili kuwasilisha na kujadili Mapendekezo ya Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Mapendekezo ya Bajeti ya Serikali na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka 2022/23.

 

3.                 Mheshimiwa Spika, naomba kuchukua fursa hii kutoa pole kwako wewe Mheshimiwa Spika, Naibu Spika, Waheshimiwa Wabunge wote, ndugu, jamaa na marafiki kwa kifo cha Mheshimiwa William Tate Olenasha aliyekuwa Mbunge wa Ngorongoro (CCM) na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu

- Uwekezaji. Mwenyezi Munguaipumzishe roho yake mahali pema peponi.

 

4.                 Mheshimiwa Spika, kwa moyo wa dhati, napenda kutoa pongezi kwa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan,Rais wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania kwa kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa busara, hekima, weledi na umahiri mkubwa pamojana kuendeleza mashirikiano na nchi mbalimbali. Tunazidi kumwombea kwa Mwenyezi Mungu aendelee kumpa nguvu, ujasirina afya njema ili aweze kuendelea kutekeleza majukumu ya kulihudumia Taifa letu kikamilifu. Aidha, naendelea kuwapongeza wasaidizi wake wakuu, kwanza Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango,Makamu wa Rais wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania pamoja na Mheshimiwa Kassim M. Majaliwa (Mb),Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kiongozi wa shughuli za Serikali Bungeni kwa kuendelea kumshauri vyema Mheshimiwa Rais.


5.                 Mheshimiwa Spika, naomba nitumiefursa hii kushukuru kumpongeza Mheshimiwa Spika pamoja na Naibu Spika kwa kuendeleakuongoza bunge letu kwa weledi. Aidha, nitumie fursas hii kuishukuru Kamati ya Kudumu ya Bajeti chini ya Mwenyekiti wake Mheshimiwa Sillo Daniel Baran, Mbunge wa Babati Vijijini (CCM) na Makamu Mwenyekiti Mheshimiwa Omari Mohamed Kigua, Mbunge wa Kilindi (CCM) kwa maoni na maboresho wakati wa vikao vya kamati. Maoni na maboreshohayo yamezingatiwa katika kuboresha Mapendekezo ya Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka 2022/23.

 

6.                 Mheshimiwa Spika, napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mheshimiwa Mhandisi Hamad Yussuf Masauni (Mb), na watendajiwote wa Wizara ya Fedha na Mipangowakiongozwa na Katibu Mkuu, Bw. Emmanuel Mpawe Tutuba kwa ushirikiano walionipa katika maandalizi ya hotuba hii, vitabu vya Mapendekezo ya Mpango na Mwongozopamoja na utekelezaji wa majukumu yangu. Aidha, ninawashukuru sana Wizara, Taasisi, Idara za Serikali, Sekta Binafsi na wadau mbalimbali waliotoa maoni na michango yao katika kukamilisha Mapendekezo ya Mpangona Mwongozo.

 

7.                 Mheshimiwa Spika, Mapendekezo ya Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka 2022/23 ni ya kwanza kwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mapendekezo haya yanawasilishwa kwenye Bunge lako Tukufu ili kupata maoni na ridhaa yaWaheshimiwa Wabunge.

 

8.                 Mheshimiwa Spika, Mapendekezo haya ni muhimu kwa kuwa yanatoa taswira ya Serikali ya Awamu ya Sita ambayo imejipambanua kwa juhudi za kuboreshamaisha ya Watanzania kwa kutekeleza mambombalimbali ikiwemo: Kuimarisha huduma za jamii hususan elimu, afya na maji kama ilivyojidhihirisha katika uzinduzi wa Kampeni ya Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano Dhidi ya UVIKO-19 uliofanyika tarehe 10 Oktoba 2021; kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara nchiniili kuchochea fursa za ajira; kuimarisha uhusiano na ushirikiano wa kimataifa; kudumisha amani na umoja wa kitaifa; na kuimarisha ulinzina usalama katikamipaka yote ya nchi. Hivyo, mapendekezo yanayowasilishwa yameainisha masuala muhimu ya kuzingatiwa na Maafisa Masuuliwa Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala wa Serikali,Sekretarieti za Mikoa, Mamlaka za


Serikali za Mitaa, Taasisi na Mashirika ya Umma wakati wa kuandaa,kutekeleza, kufuatilia, kutathmini na kutoa taarifa za utekelezaji wa Mipango na Bajeti za Mafungu yao ili kufikiamalengo ya kiuchumina kijamii yaliyobainishwa katika vipaumbele vya Taifa. Aidha, mapendekezo haya yanawasilisha vipaumbele vya Serikali katika mwaka2022/23.

 

9.                 Mheshimiwa Spika, Mapendekezo ya Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka 2022/23yamezingatia mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa Mwongozo wa mwaka 2021/22 pamoja na Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2016/17– 2020/21. Vilevile,Mapendekezo yameandaliwa kwa kuzingatia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025; Ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika kipindi cha Mwaka 2020 hadi 2025; Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Miaka Mitano(2021/22  – 2025/26); Hotuba mbalimbali za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassanikiwemo hotuba aliyoitoakatika Bunge la

12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Aprili 2021 na hotuba aliyoitoa tarehe 10 Oktoba 2021 wakati akizindua Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO-19 chini; Sera na Mikakati mbalimbali ya Kisekta pamoja na makubaliano ya kikanda na kimataifa yaliyoridhiwa na Tanzania.

 

10.            Mheshimiwa Spika, Mapendekezo haya yameainisha masualambalimbali, ikiwemo: mapitio ya utekelezaji wa mpango na bajeti kwa mwaka 2020/21 na robo ya kwanza ya mwaka 2021/22; mwenendo na mwelekeo wa hali ya uchumi; makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2022/23; maeneo ya vipaumbele vya Mpango na Bajeti kwa mwaka 2022/23; vihatarishi vya ukuaji wa uchumi na utekelezaji wa mpango na bajeti na mikakati ya kukabiliana navyo; na maelekezoyanayotakiwa kuzingatiwa na Maafisa Masuuli wakati wa uandaaji, utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini ya mpango na bajeti kwa mwaka 2022/23.


2.0            MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA MPANGONA BAJETI

 

2.1            Mwenendo wa Viashiria vya Uchumi

11.            Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2020, uchumiulikua kwa asilimia

4.8 ikilinganishwa na matarajio ya asilimia 5.5 kwa kipindi hicho na ukuaji halisi wa asilimia 7.0 mwaka 2019. Kupungua kwa kasi ya ukuaji wauchumi kulitokana na athari za UVIKO-19. Pamoja na kupungua kwa kasi ya ukuaji, Tanzania iliweza kuwa miongoni mwa nchi chache duniani zilizokuwa na ukuaji chanya wa uchumi katika mwaka 2020. Hali hii ilitokana na hatua ya Serikali ya kutositisha shughuli za biashara na uzalishaji wakati wa mlipuko wa UVIKO-19 (isipokuwa kwa kipindi kifupi tu cha robo ya pili ya mwaka 2020 ambapo baadhi ya shughuli zinazohusisha mikusanyiko ya watu kama shule, sanaa na burudani zilisitishwa kwa muda). Shughuli za kiuchumi zilizokuwa na ukuaji mkubwa mwaka 2020 ni pamoja na ujenzi (asilimia 9.1); habari na mawasiliano (asilimia 8.4); na usafirishaji na uhifadhi mizigo (asilimia 8.4). Aidha, sekta ya kilimo iliendelea kuwa na mchango mkubwa katika Pato la Taifa mwaka 2020, ikichangia asilimia 26.9, ikifuatiwa na ujenzi (asilimia 14.4), biashara (asilimia8.7), viwanda (asilimia8.4) na uchukuzi(asilimia 7.5). Mfumuko wa bei ulikuwa asilimia 4.0 Septemba 2021, ikilinganishwa na asilimia3.1 Septemba 2020.

 

12.            Mheshimiwa Spika, sekta ya nje iliathirika moja kwa moja na athari za UVIKO-19, hususan shughuli za usafiri wa anga na utalii. Katika kipindi cha mwaka ulioishia Juni 2021, urari wa malipo ya kawaida ulikuwa na nakisi ya dola za Marekani milioni 1,414.2 ikilinganishwa na nakisi ya dola za Marekanimilioni 1,127.0 katika kipindi kama hicho mwaka 2020. Akiba ya fedha za kigeni imeendelea kuwa ya kutosha mahitaji ya uagizaji wa bidhaa na huduma nje ya nchi. Hadi Juni 2021, kulikuwa na akiba ya fedha za kigeni ya dola za Marekani bilioni 5.2, ambayo inatosha kuagiza bidhaa na huduma nje ya nchi kwa kipindicha miezi 6.1. Kiwango hiki ni zaidi ya lengo la nchi la kukidhimiezi 4.0 na zaidi ya lengo la miezi 4.5 kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

 

13.            Mheshimiwa Spika, viashiria vya sekta ya benki vilikuwana mwenendo wa kuridhisha ambapo thamani ya rasilimali za benki iliimarika kama inavyojidhihirisha katika kupungua kwa mikopo chechefukufikia asilimia

9.30 Juni 2021 kutoka asilimia10.84 Juni 2020; kuongezeka kwa faida kutokanana uwekezaji wa rasilimali kutokawastani wa asilimia2.19 mwaka


2019/20 na kufikia wastani wa asilimia 2.42 mwaka 2020/21; na kuongezeka kwa faida kutokana na uwekezaji wa mtaji kutoka wastani wa asilimia 9.88 mwaka 2019/20 na kufikia wastaniwa asilimia 10.47 mwaka 2020/21.Mwenendo huu unaonesha kuendelea kuimarika kwa sekta ya benki ambapo kumekuwa na mtaji na ukwasi wa kutosha kukidhi mahitaji ya kila siku ya wenye amana na wakopaji.Kadhalika, riba za mikopo zilipungua kufikia wastani wa asilimia 16.60kutoka wastani wa asilimia16.80 mwaka 2020.

 

14.            Mheshimiwa Spika,shilingi ya Tanzaniaimeendelea kuwa imara dhidi ya sarafu za washirika wakuu wa biashara ulimwenguni katika kipindi chote cha mwaka 2020/21. Hali hii imechangiwa na: utulivu wa bei nchini;utekelezaji wa sera thabiti za fedha na bajeti; usimamizi imara katika soko la kubadilisha fedha za kigeni; kuimarika kwa urari wa biashara; na utulivu wa bei ya mafuta katika soko la dunia. Katika kipindi hicho, dola moja ya Marekani ilibadilishwa kwa wastani wa shilingi 2,309.58, ikilinganishwa na wastani wa shilingi 2,301.30katika kipindi kama hicho mwaka 2019/20. Badiliko hilo lilikuwa la kiasi cha asilimia 0.40 kwa mwaka ikilinganishwa na asilimia 0.36 katika mwaka uliopita. Kiwangohicho kilikuwa kidogona kuifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi chache duniani zilizoweza kuwa na utulivu wa kiwango cha kubadilisha fedha dhidi ya fedha za kigeni licha ya athari za UVIKO-19.

 

15.            Mheshimiwa Spika, Deni la Serikali lilifikia shilingi bilioni 64,497.83 Juni 2021 ikilinganishwa na shilingi bilioni56,449.8 Juni 2020, sawa na ongezeko la asilimia 14.3. Kati ya kiasi hicho, deni la nje ni shilingi bilioni 45,563.5 na deni la ndani ni shilingi bilioni 18,934.3. Mwenendo huo wa deni umetokana na kupokelewa kwa mikopo yenye masharti nafuu na ya kibiashara kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo hususan inayochochea ukuaji wa uchumi. Pamoja na kuongezeka kwa deni la Serikali, deni hilo limeendelea kuwa himilivu katikamuda mfupi, kati na mrefu.

 

16.            Mheshimiwa Spika, maelezo ya kina kuhusu mwenendo wa viashiria vya uchumi yanapatikana katika Sehemu ya Kwanza, Sura ya Kwanza ya kitabu cha Mapendekezo ya Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2022/23 na Sura ya Pili ya Kitabu cha Mapendekezo ya Mpango.


2.2            Utekelezaji wa Mpango na Bajeti

 

2.2.1     Utekelezaji wa Bajetiya Mwaka 2020/21

17.            Mheshimiwa Spika, Katika mwaka 2020/21, Serikaliimekusanya shilingi bilioni 31,280.1 sawa na asilimia 89.7 ya lengo. Kati ya kiasi hicho, shilingi bilioni 20,594.6 ni mapato ya ndani na shilingi bilioni 10,685.5 ni misaada na mikopo ya ndani na nje ya nchi. Aidha, Serikali ilitumia shilingi bilioni31,280.1 kugharamia shughulimbalimbali, ambapo shilingibilioni 20,613.0 ni matumizi ya kawaida na shilingi bilioni 10,667.1 ni matumizi ya maendeleo.

 

2.2.2     Utekelezaji wa Bajeti kwa Robo ya Kwanza ya Mwaka 2021/22

18.            Mheshimiwa Spika,katika robo ya kwanza ya mwaka 2021/22,jumla ya shilingibilioni 8,419.3 zilikusanywa kutoka vyanzo vyote, sawa na asilimia

93.3 ya lengo la kipindi hicho. Kati ya fedha hizo, mapato ya ndani yalifikia shilingi bilioni 5,492.1 sawa na asilimia 89.0 ya lengo la kipindi hicho. Misaada na mikoponafuu kutoka kwa Washirika wa Maendeleo ilikuwashilingi bilioni

534.4 sawa na asilimia 88.6 ya lengo. Mikopo ya kibiashara kutoka katika soko la ndani ilifikia shilingibilioni 1,220.9 sawa na asilimia117.0 ya lengo la shilingi bilioni 1,043.2. Mikopo ya ndani ilivuka lengo katika robo husika kutokana na mwitikio mzuri wa wawekezaji, hususan katika hatifungani za muda mrefu. Hata hivyo, Serikali itahakikisha kwamba ukomo uliowekwa kwa mwaka 2021/22 unazingatiwa ili kutoathiri upatikanaji wa mikopo kwa sekta binafsi. Kadhalika, mikopo ya nje ilifikia shilingibilioni 1,171.9 sawa na asilimia

96.7 ya lengo la shilingi bilioni1,211.6 katika kipindihicho.

 

19.            Mheshimiwa Spika, ridhaa za matumizi zilizotolewa katika kipindi cha robo ya kwanza kwa mwaka 2021/22 ni shilingi bilioni 8,065.6 sawa naasilimia 89.3 ya lengo la shilingi bilioni 9,028.7. Kati ya kiasi hicho, shilingi bilioni 5,517.7 ni matumizi ya kawaida na shilingi bilioni 2,547.9 ni fedha za maendeleo. Aidha, fedha za matumizi ya kawaida zilizotolewa zinajumuisha: shilingi bilioni 2,053.0 kwa ajili ya mishahara; shilingi bilioni 1,935.6 kwa ajili ya kugharamia deni la Serikali; na shilingi bilioni 1,529.2 kwa ajili ya matumizi mengineyo. Fedha za maendeleozilizotolewa zinajumuisha shilingibilioni 2,367.2 fedha za ndani na shilingi bilioni 180.7 fedha za nje. Vilevile, kiasi cha shilingi bilioni 353.7 ni fedha za Washirika wa Maendeleo zilizopelekwa moja kwa moja kwenye utekelezaji wa miradi.


20.            Mheshimiwa Spika, maelezo ya kina kuhusu Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya mwaka 2020/21na robo ya kwanza ya mwaka 2021/22yanapatikana katika Sehemu ya Kwanza, Sura ya Pili ya kitabu cha Mwongozo.

 

2.3 Utekelezaji wa Baadhi ya Miradi ya Maendeleo kwa Mwaka 2020/21 na Robo ya Kwanza ya Mwaka 2021/22 na Mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita

21.            Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2020/21 na robo ya kwanza ya mwaka 2021/22 Serikali iliendelea kutekeleza miradi ya kielelezo na shughuli nyingine katika maeneo ya kipaumbele yaliyobainishwa katika Mpangowa Tatu wa Maendeleo wa Miaka Mitano 2021/22 - 2020/21. Hatua iliyofikiwa ambayo ni sehemu ya mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita ni kama ifuatavyo:

(i)                Kukuza Mapato: Kuendelea kuimarika kwa mapato ya ndani (ikijumuisha mapato ya Halmashauri) ambapo makusanyo halisi yalikua kwa asilimia 7.2 kati ya Aprili hadi Septemba 2021 kufikia shilingibilioni 10,629.4 ikilinganishwa na shilingi bilioni 9,915.0 katika kipindi kama hicho mwaka 2020;

 

(ii)              Kulipa madeni na madai:Serikali imelipa madeniyaliyohakikiwa ya jumlaya shilingi bilioni516.23. Kati ya kiasi hicho,shilingi bilioni 111.41ni madeni ya watumishi, shilingi bilioni 70.49 ya wazabuni, shilingi bilioni 2.17 ya watoa huduma, shilingi bilioni 264.23 za wakandarasi na madeni mengineyo (madeni yanayotokana na hukumu za mahakama na fidia) yalikuwa shilingi bilioni 67.93;

 

(iii)            Kutatua kero za Muungano:Serikali imetatua changamoto 11 za Muunganozikiwemo: masuala ya usimamizi wa ukusanyaji wa mapato; ukokotoaji wa kodi kwenye huduma za simu inayofanywa na Mamlaka ya Mapato Zanzibar; na suala la ucheleweshaji wa mikataba mbalimbali ya miradi ya maendeleo;

 

(iv)            Kukuza Biashara na Uwekezaji: Kurahisisha upatikanaji wa vibali vya kazi kwa kuanzisha mfumo wa kielektroniki wa e-permit ambapo kwa sasa vibali vinapatikana kati ya siku 1 hadi 3 kutoka siku 14; kuanzishwa kwa dirisha moja la kielektroiniki la uwekezaji; kuanzishakituo cha mawasiliano cha uwekezaji na kanzidata ya ardhi yenye ukubwa wa hekta milioni1.6;


kufanyika kwa mkutano wa Baraza la Taifa la Biashara; kusajili miradi 182 yenye thamani ya dola za Marekani bilioni 3.5 inayotarajiwa kuzalisha ajira 43,782 ikilinganishwa na miradi yenyethamani ya dola za Marekanimilioni

647.43 mwaka uliopita; kutolewa kwa leseni za BRELA 6,051; kuondolewa vikwazo visivyo vya kiforodha kati ya Tanzania na Kenya kutoka 64 hadi 46; na kuridhiwa kwa mkataba wa Eneo huru la biashara Afrika (Africa Continental FreeTrade Area);

 

(v)              Kilimo: Kuzalishwa kwa mbegu bora tani 50,589.43 na miche 13,568,422 ya mazao mbalimbali; kupatikana kwa mbolea tani 678,017; na kununuliwa kwa lita 113,066 za viuatilifu vya kudhibiti visumbufu vya milipuko. Katika mwaka 2020/21, shilingi bilioni 79.9 zimetumika na katika robo ya kwanza ya mwaka 2021/22, shilingi bilioni 76.8 zimetumika.

 

Mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita katika sekta ya kilimo ni pamoja na: Kuendelea kuimarika kwa sekta ya kilimo ambapo mashamba yenye ukubwa wa hekta 237,941.9 yamehakikiwa na kupimwa afya ya udongo;ujenzi wa vihenge;ukarabati na ujenzi wa skimu za umwagiliaji; kudhibiti nzige katika mikoa ya kaskazini; kufungua vituo vya mazao nje ikiwemo katika nchi za Kenya, Sudani Kusini, China, India, Ukraine, Saudi Arabia, Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya Nchi za Afrika ya Kusini (SADC); kuimarisha hifadhi ya chakula nchini ambapo shilingibilioni 129 zilitolewa kwa Wakala wa Uhifadhi wa Chakula (NFRA) na Bodi ya Mazao Mchanganyiko; kuimarika kwa bei za mahindi kwa wakulima ambapo Serikali ilinunua mahindi kwa shilingi 500 kwa kilo kutoka bei ya shilingi 300. Hali hiyo ilipelekea kuwa na ziada ya mahindi tani 950,000; kupatikana kwa masoko ya mbogamboga na matunda aina ya parachichi nchini Qatar; na kuanza kwa ujenzi wa kiwanda cha mbolea mkoani Dodoma kinachojengwa na kampuni ya Itracom Fertilizer Ltd kinacholenga kuimarisha upatikanaji wa mbolea nchini;

 

(vi)            Mifugo: Kujengwa kwa majosho 49 katika Halmashauri 18 ambapo utekelezaji umefikia wastani wa asilimia 60; kuhimilishwa kwa ng’ombe 78,575katika mikoa 10; na kukamilika kwa ukarabati wa mabwawa matatu

(3) ya Chamakweza (Chalinze), Kimokoua (Longido) na Narakauo (Simanjiro). Katika mwaka 2020/21, shilingi bilioni 10.5 zimetumika na katika robo ya kwanza ya mwaka 2021/22, shilingi milioni 186.8. Aidha, serikali ya awamu ya


sita imefanikisha kuzinduliwa kwa viwanda vipya sita vya kusindika maziwa ikiwemo Dodoma Halisi (Dodoma), Mabuki mini-dairy (Shinyanga), Misenani mini-dairy (Mwanza) na Mbeya milk (Mbeya); kupatikana kwa masoko ya bidhaa za nyama ya mbuzi, kondoo na ng’ombe nchini Saudi Arabia pamoja na visiwa vya Comoro;

 

(vii)          Uvuvi: Kujengwa kwa ofisi tano (5) za Vikundi vya Usimamizi Shirikishi wa Rasilimali za Uvuvi (BMUs) katika Halmashauri tano (5) za Bagamoyo, LindiVijijini, Mkinga, Pangani na Chalinze; kujengwa kwa maabara moja (1) ya Utafiti ya Uvuvi katika kituo cha TAFIRI, Dar es Salaam; na kuendelea na maandalizi ya ujenzi wa Bandari ya Uvuvi na ununuzi wa meli za uvuvi katika bahari kuu. Katika mwaka 2020/21, shilingi bilioni 6.8 zimetumika na katika robo ya kwanza ya mwaka 2021/22, shilingi bilioni 2.1 zimetumika. Mafanikio mengine ni kukamilika kwa kituo cha ukuzaji viumbe bahari, samaki, mwani, majongoo ya bahari, na kamba miti (kunduchi); kupatikana kwa masoko ya mabondo ya samaki nchini China; na kutenga shilingi bilioni 50 kwa ajili ya kuanza ujenziwa bandari ya uvuvi Kilwa Masoko (Lindi);

 

(viii)        Uendelezaji wa Viwanda: Kujengwa kwa mtambo wa kuyeyusha chuma (Galvanizing Plant) katika kiwanda cha Kilimanjaro Machine Tools Company (KMTC) ambapo ujenzi umefikia asilimia 80; na kuanza kwa uzalishaji katika Kiwandacha Kuunganisha Magari cha GF Trucks Motors katika eneo la Viwanda TAMCO - Kibaha ambapo jumla ya magari 245 yameunganishwa. Katika mwaka 2020/21, shilingi bilioni 46.4 zimetumika. Aidha, Serikali ya awamu ya sita imefanikisha kutolewakwa leseni kwa kampuni 18 kupitia EPZA; kuanzishwa kwa viwanda vidogo 374; na kuanza kwa utekelezaji wa mradi wa Industrial Trade and Logistics Centre - Kurasini;

 

(ix)            Madini: Kukamilika kwa ujenzi wa Kituo cha Pamoja (One Stop Centre) Mirerani; kuanzishwa kwa masoko mapya matatu (3) ya madini ya Kiteto (Manyara), Mirerani (Arusha) na Mangaka (Mtwara); kuanzishwa kwa vituo vipya 18 vya ununuzi wa madini; kujengwa kwa makao makuu ya Tume ya Madini; kununuliwa kwa mtambo mmoja (1) wa uchorongaji (DrillRig) kwa ajili ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO); kukusanywa kwa mapato yasiyo ya kodi kiasi cha shilingi bilioni 588.04 kwa mwaka 2020/21; kununuliwa kwa vifaa vya utafiti wa jiosayansi kwa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania; na kuendelea na ujenzi wa vituo vitatu (3) vya umahiri vya Chunya, Songea na Mpanda. Katika mwaka 2020/21, shilingi bilioni 19.7 zimetumika na katika robo ya kwanzaya mwaka 2021/22,shilingi milioni 302.1 zimetumika;


 

Aidha, Serikali ya awamu ya sita imefanikisha kutolewa kwa leseni za uchimbaji madini 5,126 ikilinganishwa na 3,195 katika kipindi kama hicho mwaka uliopita; kukusanywa kwa mapato ya jumla ya shilingi milioni 336.5; ujenzi wa kiwanda cha kisasa cha kusafisha dhahabu Mwanza chenye uwezo wa kusafisha kilo 480 kwa siku; na kufutwa kwa Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa wafanyabiasha watakaoleta dhahabu kwenye viwanda vya ndani;

 

(x)              Utalii: Kuanza kuimarika kwa sekta ya utalii ambapo watalii waliotembelea nchini wamefikia 464,913; na kuanzishwa kwa mpango wa kutangaza utalii nchini ikiwemo kipindi cha Royal Tour kinacholenga kutangaza vivutio vya utalii na fursa za kiuchumi nchini. Kadhalika katika utekelezaji wa miradi mahususi chini ya kampeni ya maendeleo na mapambano ya UVIKO 19, Shilingi bilioni 90.2 zimeelekezwa kugharamia sekta ya utalii ambayo iliathirika na UVIKO-19 baada ya mataifambalimbali duniani ambao ni washirikawetu kibiashara kuchukuahatua za kudhibitikuenea kwa maambukizi ya UVIKO-19 ikiwemo kusitisha usafiri wa anga, na kuzuia watu kusafiri (wakiwemowatalii). Fedha hizo zitatumika kutekeleza yafuatayo:Kuimarisha taasisi za sekta ya utalii zilizoathiriwa kwa kiasi kikubwana UVIKO-19 zikiwemoTANAPA, TAWA na NCAA, TFS na NMT ikiwemo kuboresha miundombinu katika maeneo ya hifadhi na maeneo yanayozunguka hifadhi hizo kwa kukarabati barabara na kununua mitambo mitano (5) kwa ajili ya kujenga na kukarabati miundombinu hiyo katika hifadhi 13 za Taifa; Kuimarisha mifumo ya utangazaji wa fursa za utalii; Kubaini na kuwezesha ulipaji fidia kwa kodi na tozo zenye madhara makubwa kwa wafanyabiashara wa utalii kwa maeneo ya hifadhi za Taifa katika kipindi hiki cha UVIKO -19; na Kuanzisha vituo vitatu vya ukusanyaji maduhuli ambavyo vinajumuisha ujenzi wa malangoya kupokelea wageni katika maeneo yaliyopo katika hifadhi;

 

(xi)            Reli ya Kati: Ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha Kimataifa (Standard Gauge Railway- SGR) wa kipande cha Dar es Salaam – Morogoro (km 300)umefikia asilimia 93 na Morogoro – Makutupora Singida (km 422) umefikia asilimia 70; na kuanza kwa ujenzi wa kipande cha Mwanza – Isaka (km 341). Katika mwaka 2020/21, shilingi bilioni 1,726.53 zimetumika na katika robo ya kwanzaya mwaka 2021/22,shilingi bilioni 79.3 zimetumika;


(xii)          Kuboresha Usafiri wa Abiria na Mizigo katika Maziwa Makuu: Ziwa Victoria: Kukamilika kwa ukarabati wa meli mbili (2) za New Butiama Hapa Kazi Tu na New Victoria Hapa Kazi Tu; kuendelea na ujenzi wa meli mpya ya MV Mwanza Hapa kazi Tu ambao umefikia asilimia 80.1; na kukamilika kwa ujenzi wa chelezo cha kujengea na kukarabati meli katika Bandari ya Mwanza. Ziwa Tanganyika: kusainiwa kwa mikataba kwa ajili ya ujenzi wa meli mpya na ukarabati wa meli ya MT. Sangara. Ziwa Nyasa: kukamilika kwa ujenzi wa matishari mawili (2) yenye uwezo wa kubeba tani 1,000 kila moja; na kukamilika kwa ujenzi wa meli moja mpya ya MV Mbeya II. Katika mwaka 2020/21, shilingi bilioni 48.5 zimetumika na katika robo ya kwanza ya mwaka 2021/22, shilingi bilioni 4.9 zimetumika;

 

(xiii)        Usafiri wa anga: Kuanza ujenzi wa uwanja wa ndege wa Msalatona kusainiwa kwa mikataba ya ujenzi wa viwanja vya ndege vya mikoa ya Shinyanga, Tabora,Sumbawanga pamoja na kuanza maandalizi ya maboresho ya kiwanja cha ndege cha Kigoma; kuendeleana ujenzi wa viwanja vya ndege vya Songea (asilimia 95), Mtwara (asilimia 61) na Iringa (asilimia 21.3); kukamilisha malipo ya awamu ya mwisho na kupokelewa kwa ndege tatu hivyo kufanya jumla ya ndege mpya zilizonunuliwa kufikia 11; Shirika la Ndege la Tanzania kupata kibali cha kwenda moja kwa moja nchi mbalimbali ikiwemo Falme za Kiarabu; na kusainiwa mkataba wa ununuzi wa ndege tano ambapo shilingi bilioni596.3 zimetolewa;

 

(xiv)        Barabara na Madaraja: Mtandao wa barabara nchini umefikia kilomita36,361.95 ambapo barabara kuu ni kilomita 12,215.58 na barabara za mikoa ni kilomita 24,146.37; na ujenzi wa madaraja 8,647 katika barabara kuu na za mikoa. Katika kipindi cha mwaka 2020/21 shilingi bilioni 1,552.8 zimetumika na katika robo ya kwanza ya mwaka 2021/22, shilingibilioni 295.8 zimetumika. Mafanikio mengine ya awamu ya sita ni pamoja na kuanza ujenzi wa barabaraza kupunguza msongamano wa vyombo vya moto mkoani Dodoma. Barabara hizi ni pamoja na ujenzi wa barabara ya mzunguko katika jiji la Dodoma (Dodoma outer ring road) yenye urefu wa kilometa (112.3) ambapo ujenzi umeanza na unatarajiwa kukamilika 2023. Kazi nyingine ni maandalizi ya upanuzi wa barabara kutoka Dodoma kwenda Singida (km 50),Dodoma – Iringa (km 50), Dodoma – Arusha (km 50) na Dodoma – Morogoro (km 70); kuendelea kwa ujenzi wa barabara ya njia nane Kimara – Kibaha ambapo ujenzi umefikia takribanasilimia 95; kuendeleana ujenzi wa madaraja makubwa ya Tanzaniteasilimia 97, Kigongo– Busisi asilimia 32 na


Wami asilimia 65. Aidha, maandalizi ya ujenzi wa barabara ya ndani ya jiji la Dodoma (Dodoma inner ring road; km 6.4) yanaendelea chini ya ufadhili wa Serikali ya Japan.

 

Shilingi bilioni 228.3 zilitolewa katika robo ya kwanza ya mwaka 2021/22 kwa ajili ya ujenzi wa barabara za mijini na vijijini ambapo kazi zilizokamilika ni ujenzi wa barabara za lami kilomita 27.1, barabara za changarawe kilomita 21.6, madaraja/Vivuko 62 na matengenezo ya barabara zenye urefu wa kilomita 4,439.28. Vilevile, shilingi bilioni 1.5 zimetolewa kwa kila jimbo kwa ajili ya uwekajiwa lami kwenye barabara za miji.

 

Katika hatua nyingine, Serikali inatarajia kuanza ujenzi wa barabara mpya za kufungua fursa za kiuchumizenye urefu wa kilomita 879 katika sehemu mbalimbali nchini.Hii itasaidia kufunguazaidi Taifa kama kituo cha uzalishaji, biasharana usafirishaji kikanda.Aidha, Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) na Mshauri Elekezi inakamilisha mchoro (design) wa daraja la Jangwani ili kufanikisha maandalizi ya majadiliano baina ya Benki ya Dunia na Serikali ya ufadhili wa ujenzi wa daraja hilo unaotarajiwa kuanza kutekelezwa mwaka 2022/23.

 

(xv)          Uendelezaji wa Bandari: Bandari ya Dar es Salaam: Awamu ya kwanza utekelezaji umefikia asilimia 95 ambapo gati Na. 1 – 7 limeongezwa kina hadi kufikia mita 14.5 na gati maalumu ya kuhudumia meli za magari (RoRo) limeanzakutumika. Katika mwaka 2020/21, shilingibilioni 124.4 zimetumika na katika robo ya kwanzaya mwaka 2021/22,shilingi bilioni 2.4 zimetumika;

Bandari ya Mtwara: Ujenzi wa gati moja (1) lenye urefu wa mita 300 na sakafu ngumu umekamilika ambapo katika mwaka 2020/21, shilingi bilioni 65.47zimetumika; na

 

Bandari ya Tanga: Uongezaji wa kina cha lango la bandari kutoka mita 4 hadi mita 13 na ujenzi wa gati mbili (2) kwenye kina kirefu umekamilika. Katika mwaka 2020/21, shilingi bilioni 20.41 zimetumika na katika robo ya kwanzaya mwaka 2021/22,shilingi bilioni 11.6 zimetumika.

 

(xvi)     Nishati

Miradi ya umeme:Utekelezaji wa Mradi wa Kufua Umeme wa Maji -


Julius Nyerere MW 2,115 umefikia asilimia 55.6, ambapo ujenzi wa handaki la kuchepushia maji umekamilika. Aidha, kazi nyinginezinazoendelea ni pamoja na: ujenzi wa tuta kuu la bwawa; ujenzi wa njia za kupeleka maji kwenye mitambo; ujenzi wa jengo la mitambo; kingo za bwawa (Saddle Dams); kituo cha kuongeza nguvu ya umeme - Switch Yard; na utengenezaji wa mitambo tisa (9) ya kuzalisha umeme (turbinesand generators) yenye uwezo wa kuzalisha MW 235 kila mmoja. Katika mwaka 2020/21, shilingi bilioni 1,171.53 zimetumika na katika robo ya kwanza ya mwaka 2021/22,shilingi bilioni 81.4 zimetumika. Miradi mingine ni:Kuendelea na usambazaji umeme vijijini ambapo jumla ya vijiji 10,361 kati ya vijiji 12,317 vya Tanzania Bara sawa na asilimia84.12 vimeunganishiwa umeme; mradi wa Rusumo MW 80 umefikia asilimia 81.2; Mradi wa Njia ya Kusafirisha Umeme msongo wa KV 220 kutoka Bulyanhulu hadi Geita yenye urefu wa kilomita 55 umekamilika. Miradi hii katika mwaka 2020/21 imetumia jumla ya shilingi bilioni 1,067.0 na katika robo ya kwanza ya mwaka 2021/22, shilingi bilioni 88.1 zimetumika.

 

Mafanikio mengine ni: kuendelea na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Rufiji - Chalinzeambapo shilingi bilioni112.9 zimetumika; kuendelea na ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ya Singida - Arusha - Namanga ambapo utekelezaji umefikia asilimia 96.1; na miradi ya Ruhudji na Rumakali imepata ufadhili kupitia Serikali ya China;

 

Mradi wa Ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi: Hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima (Uganda) hadi Chongoleani - Tanga (Tanzania) - EACOP ni kuanza kwa taratibu za ujenzi wa mradi baada ya kukamilika kwa majadiliano na kusainiwa kwa Mkataba kati ya Nchi Hodhi na Wawekezaji (Host Government Agreement – HGA) na Mkataba wa Ubia (Shareholding Agreement – SHA). Katika mwaka 2020/21,shilingi bilioni 262.7 zimetumika kwa ajili ya ununuzi wa sehemu ya hisa za Serikali, sawa na asilimia 45.4 ya lengo la mtaji washilingi bilioni 577.7;

 

Mradi wa Kuchakata na Kusindika Gesi Asilia – Lindi: Kukamilika kwa ulipaji wa fidia kwa wananchi waliopisha mradi katika maeneo ya Likong’o na Masasi ya Leo. Katika kipindi cha mwaka 2020/21shilingi


bilioni 2.6 zimetumika;

 

(xvii)      Afya: Kuendelea na ukamilishaji wa ujenzi na ukarabati wa hospitali za rufaa za mikoa 19; kuendelea na ujenzi wa Hospitali 99 za Halmashauri ambazo zipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji; kutolewa chanjo kwa watoto 2,112,411 wenye umri wa chini ya miaka mitano, sawa na asilimia 101 ya lengo la watoto 2,091,378; upatikanaji wa dawa muhimu katika vituo vya kutolea huduma za afya umefikia asilimia 94; kununuliwa kwa mashine za X- ray 11 za kidigitali ambazo zimesambazwa katika hospitali za mikoa 11; na kufungwa kwa mitambo 19 ya kuzalisha hewa ya Oksijeni katika hospitali za rufaa za mikoa. Katika mwaka 2020/21, shilingi bilioni 402.7 zimetumika na katika robo ya kwanza ya mwaka 2021/22, shilingi bilioni 83.2 zimetumika. Aidha, Serikaliimepata dozi 1,058,000za chanjo ya UVIKO-19 aina ya Johnson and Johnson kutoka USA na dozi 1,065,000 aina ya Sinopham kutoka COVAX facility ambapo hadi tarehe 20 Oktoba, 2021 jumla ya watu 959,377 ambao ni sawa na asilimia 90.6 walipata chanjo ya JJ na watu 8,591 walipata chanjo aina ya Sinopham; shilingi bilioni 234 zilitolewa kwa ajili ya kununua dawa na shilingi bilioni 26.3 kwa ajili ya vifaa tiba; shilingi bilioni 7.9 kwa ajili ya kununua mashine ya kupasulia ubongo bila kupasua kichwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete; kuendelea na utekelezaji wa miradi 25 ya hospitali za rufaa za mikoa na kanda ambapo shilingi bilioni 159 zimetolewa; na kujengwa kwa vituo vya afya katika tarafa 221 ambapo shilingi bilioni 37.5 zimetolewa; Kadhalikakatika utekelezaji wa miradi mahususichini ya kampeni ya maendeleo na mapambano dhidi ya UVIKO 19 katika sekta ya afya, shilingibilioni 466.9zimepelekwa kwa ajili ya:

(i)                Kujenga na kukarabati miundombinu ya vyumba vya wagonjwa

mahututi (ICU) katikahospitali 67;

(ii)              Kununua vifaa katikaICU za hospitali 66;

(iii)            Kujenga na kukarabati Miundombinu ya kutolea Huduma za Dharura(EMD) katika hospitali 115;

(iv)            Kununua vifaa katika miundombinu ya kutolea hudumaza dharura za hospitali 119;

(v)              Kununua magari 253 ya kubeba wagonjwa (20 yenye kiwango cha huduma za juu - advanced ambulance na magari 233 yenye kiwango cha huduma ya msingi - basic ambulance);

(vi)            Kusimika mfumo wa usambazaji wa hewa tiba ya Oksijeni kwa wagonjwa katika wodi za hospitali 82;


(vii)          Kununua mitungi 5,782 ya hewa tiba ya Oksijeni na vifaa wezeshi vya utoajihewa tiba katika hospitali 116;

(viii)        Kusimika mitambo tisa (9) ya kuzalisha hewa tiba;

(ix)            Kununua vifaa wezeshi vya utoaji (flowmeters) hewa tiba katika Hospitali 116;

(x)              Kununua seti 2,700 za vitanda vya wagonjwa vyenye godoro, kabati na meza;

(xi)            Kununua na kusimika mashine 85 za X-ray, CT-Scan 29, mashine saba (7) za huduma za uchunguzi wa moyo (Echo Cardiography) na MRI nne (4);

(xii)          Kununua mashine za upimaji gesi katika damu, vitendanishi vya upimaji wa UVIKO -19 na mashine za uchambuaji wa mazao ya damu salama;

(xiii)        Kugharamia uingizaji, utunzajina usambazaji wa chanjo;

(xiv)        Kuelimisha na kuhamasisha jamii kuhusu chanjo ya UVIKO;

(xv)          Kununua magari 214 kwa ajili ya huduma za chanjo katika mikoa na halmashauri na kampeni za kuhamasisha uchomajiwa chanjo;

(xvi)        Kugharamia ukarabati wa hospitalimaalum ya mirembena hospitali za rufaa za mikoa ya lindi, ligula-mtwara na kitete- tabora;

(xvii)      Kukarabati nyumba 116 za watoa huduma wa afya katika hospitali za rufaa za mikoa 26 na hospitali za wilaya 90 pamoja na kukarabati miundombinu kwenye hospitali sita (6) za Rufaa za Mikoa; na

(xviii)    Kuwajengea uwezo watumishi wa sekta ya afya kwa kuwapatiamafunzo na kugharamia tafiti mbalimbali zinazohusu UVIKO-19.

(xviii)    Elimu: Kukamilika kwa ujenzi wa miundombinu katika shule za msingi 998 na sekondari 719 kwenye Halmashauri 184; ujenzi wa maktaba saba (7) katika mikoa ya Kigoma,Rukwa, Kagera, Kilimanjaro, Morogoro, Iringa na Tabora; na ujenzi wa vyuo vya VETA vya Chato, Gorowa (Manyara), Ngorongoro, Simanjiro na Karagwe. Shughulinyingine ni kuendeleana utekelezaji wa programu ya Elimumsingi Bila Ada; na kutolewa kwa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 415 kwa wanafunzi 149,472 wa Elimu ya Juu. Katika mwaka 2020/21, shilingi bilioni 683.0 zimetumika na katika robo ya kwanza ya mwaka 2021/22, shilingi bilioni 152.9 zimetumika. Mafanikio mengine ni pamoja na kusainiwa kwa mkopo wa Benki ya Dunia wa shilingi bilioni 972 kwa ajili ya uboreshaji elimu kwenye vyuo vikuu 14; kuanza ujenzi wa chuo kikubwa cha ufundi Dodoma ambapo shilingi bilioni 18 zimetumika; na kutolewa kwa


shilingi bilioni40 kwa ajili ya ujenzi wa vyuo vya ufundi stadi katikawilaya 25.

 

Vilevile, kupitia kampeni ya maendeleo na mapambano dhidi ya UVIKO- 19, sekta ya elimu imetengewa Shilingi bilioni368.9 ambapo:Shilingi bilioni 304 zitatumika kupunguza msongamano madarasani na kwenye mabweni kwa kujenga vyumba vya madarasa 15,000 katika shule za sekondari na shule za msingi shikizi pamoja na madawati 641,850; na kujengamabweni 50 kwa ajili ya wanafunzi wenye ulemavu; na Shilingi bilioni 64.9 zitaelekezwa kukamilisha Vyuo vya Ufundi Stadi - VETA sita (6) vya mikoa na 26 vya Wilaya; kuchapisha vitabu vya nukta nundu 10,812 kwa ajili ya wanafunzi wasioona; na kugharamia vifaa kwa ajili ya wanafunzi 486 wenye mahitaji maalum katika vyuo 11;

 

(xix)        Maji: Upatikanaji wa huduma ya maji umeimarika ambapo hadi Juni, 2021 imefikia wastani wa asilimia 72.3 vijijini kutoka wastani wa asilimia 70.1 Juni, 2020 na mijini asilimia 86 kutoka asilimia 84. Kazi zilizofanyika ni pamoja na: ukarabati wa vituo 159 vya kufuatilia mwenendo wa maji; na kukamilika kwa miradi 666 iliyonufaisha wananchi 3,820,180 waishio vijijini. Katika mwaka 2020/21, shilingi bilioni 495.3 zimetumika na katika robo ya kwanza ya mwaka 2021/22, shilingi bilioni 99.8 zimetumika; Kutolewa kwa shilingi bilioni 352 kwa miradi 328 (mjini 17 vijini 311) ambapo miradi yenye thamani shilingi bilioni 109.13 imekamilika na kunufaisha wananchi 1,975,197 vijini na 372,002 mijini; na maandalizi ya mradi wa kutoa maji kutoka Ziwa Victoria hadi Dodoma. Serikali pia inaendelea na utekelezaji wa miradi mahususi chini ya kampeni ya maendeleo na mapambano dhidi ya UVIKO 19 ambapo Shilingi bilioni 139.4 zitagharamia huduma za maji safi ikijumuisha: Shilingi bilioni 101.7 kwa ajili ya ukarabati, upanuzi na uongezaji wa miundombinu ya usambazaji wa maji na Shilingi bilioni 37.6 kwa ajili ya kununua mitambo ambayo ni mitambo 25 ya kuchimba maji ili kuongeza kasi ya uchimbaji wa visima vinavyohitajika katika maeneo mbalimbali nchini, seti tano (5) za mitambo ya uchimbaji na ujenzi wa mabwawa ili kuongeza kasi ya ujenzi wa mabwawa katika maeneo yenye uhitaji; na seti nne (4) ya vifaa vya uchunguzi wa maji chini ya ardhiili kupata maeneosahihi ya kuchimbavisima;

 

(xx)          Habari, Mawasiliano na TEHAMA: Kukamilika kwa ujenzi wa mkongo wa taifa kwa kilomita 409 katika mgawanyo ufuatao: Kilomita 72 kuunganisha nchi ya Msumbiji kupitia mpaka wa Mtambaswala katika Mkoa wa Mtwara na kukamilika kwa kituo cha kutoa hudumaza mawasiliano, Kilomita72


Kuunganisha Watumiaji wa Mwisho (Last mile connectivity) katika Ofisi za Serikali na kilomita 265 Awamu ya kwanza Manyoni – Kambi Katoto (Chunya); Kukamilika kwa ukarabati wa kilomita 105 za ujenzi wa mkongo Arusha – Namanga kupitia miundombinu ya TANESCO; Ununuzi wa magari 47 kwa ajili ya kuhudumia shughuli za mkongo; kukamilika kwa uwekaji wa miundombinu ya anwani za makazi katika kata 18 ya Halmashauri ya Jiji la Mwanza; na kubandikwa kwa vibao 78,138 vya namba za nyumba katika Halmashauri ya Jiji la Mwanza.Katika kipindi cha mwaka 2020/21shilingi bilioni 16.0 zimetumika na katika robo ya kwanza ya mwaka 2021/22, shilingi bilioni 8.4 zimetumika;

 

(xxi)        Mahakama na Utawala wa Sheria: Kuimarisha Mifumo ya Utoaji Haki na Usimamzi wa Sheria ambapo jumla ya mashauri 104,441 yalisikilizwa katika ngazi mbalimbali za mahakama; kuteuliwa kwa Majaji wapya saba (7) wa mahakama ya rufaa, Majaji 21 wa mahakama kuu na kuajiriwa kwa mahakimu 245; ujenzi wa Vituo Sita Jumuishi vya Utoaji huduma za mahakama katika mikoa ya Arusha, Dar es salaam, Dodoma, Morogoro, na Mwanza; kukamilika kwa ujenzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Katavi na Mahakama za Wilaya za Bunda, Chemba na Bahi; kuanza ujenzi wa Mahakama za Mwanzo 18 katika maeneo mbalimbali nchini; kuendelea na ukarabatati wa Mahakama Kuu moja (1), mahakama mbili (2) za hakimu mkazi na tisa (9) za wilaya; kufungua Ofisi za Mashtakaza wilaya za Kilombero, Serengetina Karagwe; na kufuta Mashkata 467 yasiyo na tija. Aidha, Serikali ipo katika majadiliano na Benki yaDunia kwa ajili ya kupata fedha za kuendelea kujengana kuimarisha miundombinu ya mahakama. Kiasikilichoombwa ni dola za Marekanimilioni 75 ambazozinatarajiwa kupatikana katikamwaka huu wa fedha;

 

(xxii)      Ulinzi na Usalama: kutolewa kwa vibali vya kuajiri jumla ya askari 5,403kwa ajili ya Jeshi la Polisi (askari 4,103), Jeshi la Magereza(askari 700) Jeshi la Zimamoto na Uokoaji (askari 250) na Idara ya Uhamiaji (askari 350); Kuendeleana ujenzi wa nyumba 119 za Maafisana Askari wa Jeshi la Magereza zenye uwezo wa kuhudumia familia 210; kuendelea na ujenzi wa nyumba za makazi ya Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika eneo la Kikombo, Jijini Dodoma.

 

(xxiii)    Utumishi wa umma: Watumishi 29,900 wameajiriwa, watumishi 180,830 wamepandishwa vyeo na kulipwastahili zao, watumishi8,202 wamebadilishiwa kada, watumishi 30,228 wamelipwa malimbikizo ya madeni


ya jumla ya shilingi bilioni55.75 na kupunguza makato ya kodi ya PAYEkufikia asilimia 8 kutoka asilimia 9; na mifuko ya hifadhi ya jamii (PSSSF na NSSF) kulipa mafao ya shilingi bilioni 1,540 na pensheni shilingi bilioni 446.93. Aidha, Serikali imeanza mchakato wa kutoa hatifungani maalum zisizo taslimu (non-cash special Bonds) za miaka 8 hadi 25 kwa ajili ya kulipa madeni ya mifuko ya hifadhi ya jamii ambapo kiasi cha shilingi bilioni2,176.74 kilichohakikiwa cha deni la Pre-1999 kimeridhiwa kutolewa kuanzia Desemba2021 na deni lililobakia linaendelea kufanyiwa uhakiki;

 

(xxiv)    Kaya maskini: Kuimarisha maisha ya kaya maskini kupitia TASAF ambapo kaya 879,670 zilinufaika kwa kupatiwa jumla ya shilingibilioni 71.395; sambamba na utekelezaji wa miradi mahususi chini ya kampeni ya maendeleo na mapambanoya UVIKO 19 ambapo Shilingi bilioni5.5zitatumika kuwezesha kaya masikini 34,375 kukidhi mahitaji ya msingi kupitia TASAF ikiwepo upatikanaji wa vifaa kinga;

 

(xxv)      Kuwezesha Wajasiriamali Wadogo: Kupitia kampeni ya maendeleo na mapambano ya dhidi ya UVIKO 19, Serikali itawawezesha makundi maalum ya wajasiriamali wadogo ikijumuisha vijana, wanawake na wenye ulemavu kwa kuwajengea vibanda vya kufanyia biasharaili kupunguza msongamano usio wa lazima ambapo shilingi bilioni 5 zitatumika;

 

(xxvi)    Ardhi: Kusajiliwa kwa hati miliki 41,533 ikilinganishwa na hati miliki 34,588 katika kipindikama hicho mwaka2020; kushughulikiwa kwa migogoro ya ardhi 745 kwa njia za kiuatwalana mashauri 13,991kwa kutumia mabarazaya ardhi; kupimwa kwa viwanja 232,596 na mashamaba 353; Kutambuliwa, kupangwa na kupimwa kwa vipande 87,636 vya ardhi katika halmashauri 24; na kuandaliwa kwa mipango ya matumizi ya ardhi ya vijiji 51 vilivyopo katika mkuza wa bomba la mafuta ghafi kutoka Uganda hadi Tanga. Aidha, mashamba 11 yenye ekari 24,156 yamebadilishiwa matumizi kwa ajili ya shughuli mbalimbali ikiwemo uwekezaji.Katika mwaka 2020/21,shilingi bilioni

5.4 zimetumika na katika robo ya kwanza ya mwaka 2021/22,shilingi bilioni

2.8 zimetumika;

 

(xxvii)  Sanaa na Burudani: Kuanzishwa kwa Mfuko wa Maendeleo ambao umetengewa shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya kusaidia timu za Taifa; COSOTA kutengewabajeti ili kuiwezesha kukusanya makusanyo ya wasanii; na kufutiwa Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa nyasi bandia;


(xxviii)   Ushirikiano na Washirika wa maendeleo: Kupatikana kwa misaada na mikopo nafuu ya shilingi trilioni1.447; kusainiwa kwa mikataba 31 na Washirikawa maendeleo yenye thamaniya shilingi trilioni 6.3;

 

(xxix)       Kuimarisha diplomasia: Kufunguliwa kwa ubalozimpya wa Tanzania Vienna - Austria; kufunguliwa kwa Konseli Kuu katika miji ya Lubumbashi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Guangzhou nchini China; na kuridhiwa kwa Mkataba wa Uanzishwaji wa Eneo Huru la Biashara Africa (AfCFTA);na

 

(xxx)      Makao Makuu ya Serikali Dodoma: Hatua za kuimarisha makao makuu ya Serikali Dodoma zinaendelea ambapo vibali vya ujenzi vimetolewa na michoro ya ubunifu kwa ajili ya kuanza awamu ya pili ya ujenzi wa ofisi 22 za Wizarana Mwanasheria Mkuu wa Serikali imekamilika na kiasi cha shilingi bilioni 300 zimetengwa kwenyebajeti ya mwaka2021/22 kwa ajili ya kuanzaujenzi huo.

 

22.            Mheshimiwa Spika, maelezo ya kina kuhusu utekelezaji wa miradi ya maendeleo mwaka 2020/21 na robo ya kwanza ya mwaka 2021/22yameainishwa katika kitabucha Mapendekezo ya Mpango (Sura ya Tatu).

 

2.4 Changamoto za Utekelezaji wa Mpango na Bajeti na Hatua na Kukabiliana Nazo

23.            Mheshimiwa Spika, Utekelezaji wa Mwongozo wa mwaka 2021/22 ulikabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo: uwasilishaji wa mahitaji makubwa kuliko ukomo uliotolewa; kupungua kwa shughuli za kibiashara na kiuchumi kutokanana athari za UVIKO -19; kutoandaliwa kwa miradi inayokidhi vigezo vya kutekelezwa kwa utaratibu wa ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi; mabadiliko ya viwango vya riba katika masoko ya fedha ya kimataifa; na upungufu wa rasilimali watu hususan wahandisi wa kusimamia utekelezaji wa miradi pamoja na wataalamwa uendeshaji wa mitambo na vifaa vinavyotumia teknolojia ya kisasa.

 

24.            Mheshimiwa Spika, katika kukabiliana na changamoto za utekelezaji wa Mpango na Bajeti, Serikaliinaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kukabiliana na changamoto hizo zikiwemo: Kujenga uwezo wa Mafungu katika kuwianisha mipango na ukomo wa bajeti uliotolewa; kuendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo wa biashara duniani ili kutumia fursa zilizotokana na athari za UVIKO-19; kuchukuahatua za kiserana kiutawala kuimarisha sekta


zilizoathirika na UVIKO-19;kuendelea kujenga uwezo wa Mafunguili kuyawezesha kuandaa miradi inayokidhi vigezo vya kutekelezwa kwa utaratibu wa PPP; kuendeleakutekeleza miradi ya maendeleo yenye kuchachua shughuliza kiuchumi pamoja na kujengamazingira wezeshi ya kuvutia biasharana uwekezaji; na kuendelea kuajiriwahandisi na wataalamwatakaosimamia utekelezaji na uendeshaji wa miradi.

 

25.            Kwa kumalizia eneo hili la Utekelezaji wa Baadhi ya Miradi ya Maendeleo kwa Mwaka 2020/21na Robo ya Kwanza ya Mwaka 2021/22na Mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita naomba nisisitize mambo matatu:-

(i)          Kwa maafisa manunuzi, Maafisa Masuuli na wasimamizi wa miradi hii, tunataka uzingatiaji wa sheria na maelekezo katika utekelezaji wa miradi hii, tunataka ubora wa miradi, tunataka “Value for Money”katika miradi yote.

 

(ii)        Kwa wote wanaohusika na ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi kitengo cha M & E, Expenditure tracking, Sekretariet za mikoa yote tufuatilie miradi kila siku, sio kusubiri ziara za viongozi, wala sio kusubiri kazi iharibike. Wakaguzi wa ndani tubainishe dosari kila zinapojitokeza, kwa ambao hawataona dosari katika maeneo yao mpaka wakaguzi wa nje waje wayabainishe watakuwa wamepoteza sifa za kuwa kwenye nafasi hizo.

 

(iii)      Niwapongeze wote mnaohusika na kukusanya mapato ya Serkali.Tuendelee kuweka mkazo katika kukusanyamapato. Bado kuna ulegevu katika ukusanyaji wa mapato katika baadhi ya maeneo. Kuna UVUJAJI Mkubwa wa makusanyo ya maduhuli ya serikali katika Serikali za mitaa na ulegevu wa matumizi ya EFD (Tunashauriana bei ya risiti na isiyona risiti). Aidha, kuna vitendovya rushwa katika baadhi ya ukusanyaji wa kodi kutoka kwa walipa kodi wakubwa (tunashauriana kiasi gani kiende serikalini na kiasi gani kije mifukoni mwetu). Tuviache vitendo hivyo mara moja.


3.0    MWONGOZO WA MAANDALIZI YA MPANGO NA BAJETI YA SERIKALI KWA MWAKA 2022/23

 

26.            Mheshimiwa Spika, masuala ya msingi yatakayowezesha kufikia shabaha za uchumi jumla ni pamoja na: kuongezeka kwa ushiriki wa sekta binafsi kwenye shughuli za maendeleo; kuendelea kuhimili athari za majanga ya asili; kuimarika kwa uchumi wa dunia na utulivu wa bei katika masoko ya kimataifa; kuendelea kuwa na utoshelevu wa chakula nchini; na uwepo wa amani, usalama, umoja, utulivu wa ndani na nchi jirani.

 

27.            Mheshimiwa Spika, shabaha na malengo ya uchumi jumla yatakayozingatiwa katikamuda wa kati ni pamoja na:-

(i)          Kuongeza kasi ya ukuaji wa Pato la Taifa kutoka asilimia 4.8 mwaka 2020 hadi asilimia 5.0 mwaka 2021 na kuendeleakukua hadi asilimia

5.2 mwaka 2022;

 

(ii)        Kuendelea kudhibiti kasi ya mfumuko wa bei na kuhakikisha kuwa unabaki kwenye wigo wa tarakimu moja ya wastani wa asilimiakati ya

3.0 - 5.0 katika muda wa kati;

 

(iii)      Mapato ya ndani(ikijumuisha mapato ya Halmashauri) kufikiaasilimia

16.3 ya Pato la Taifa mwaka 2022/23 na 2023/24;

 

(iv)      Mapato ya kodi kufikia asilimia 13.8 ya Pato la Taifa mwaka 2022/23 kutoka matarajio ya asilimia 12.9 mwaka 2021/22;

 

(v)        Kuhakikisha kuwa nakisi ya bajeti (ikijumuisha misaada)haizidi asilimia

3.0    yaPato la Taifa kuendana na makubaliano ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki; na

 

(vi)      Kuwa na akiba ya fedha za kigeni kwa kiwango cha kukidhi mahitaji ya uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje kwa kipindi kisichopungua miezi minne (4).

 

3.1            Mfumo wa Awali wa Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka 2022/23

28.            Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2022/23, Serikaliinatarajia kukusanya na kutumia jumla ya shilingibilioni 39,387.5, ikilinganishwa na


shilingi bilioni 36,681.9 mwaka 2021/22. Kiasi kilichoongezeka ni sawa na asilimia 7.4 kutokana na mahitaji ya kugharamia miradi mbalimbali; ongezeko la mishahara ya watumishi wa umma; ajira mpya pamoja na fursa zilizopo za mapato ya ndani na nje. Kati ya kiasi hicho, mapato ya ndani (yakijumuisha mapatoya Halmashauri) yanakadiriwa kufikia shilingi bilioni28,567.9, sawa na asilimia 72.5 ya bajeti yote. Aidha, Washirika wa Maendeleo wanatarajiwa kuchangia shilingi bilioni 3,043.5, sawa na asilimia 7.7 ya bajeti yote. Serikali inatarajia kukopa shilingi bilioni5,354.3 kutoka soko la ndani ambazo zinajumuisha shilingi bilioni 3,300.0kwa ajili ya kulipia hatifungani na dhamana za Serikali zinazoivana shilingi bilioni2,054.3 kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo. Vilevile, mikopo ya masharti ya kibiashara kutoka nje inatarajiwa kuwa shilingibilioni 2,421.9.

 

29.            Mheshimiwa Spika, kwa upande mwingine, Matumiziya Serikali yanakadiriwa kufikia shilingi bilioni 39,387.5, ambapo shilingi bilioni 24,708.6 ni matumizi ya kawaida na shilingi bilioni 14,678.9 ni matumizi ya maendeleo. Kati ya fedha za matumizi ya maendeleo, shilingi bilioni 11,635.4 ni fedha za ndani na shilingi bilioni 3,043.5 ni fedha za nje.

 

30.            Mheshimiwa Spika, maelezo ya kina kuhusu sera za mapato na matumizi katika muda wa kati yapo katika Sehemu ya Kwanza, Sura ya Tatu ya Kitabu cha Mwongozo.

 

3.2            Maelekezo Mahsusi ya Mwongozo

31.            Mheshimiwa Spika, Mwongozo wa Mpango na Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2022/23 umeainisha maelekezo mbalimbali ambayo Maafisa Masuuli watatakiwa kuyazingatia wakati wa uandaaji, utekelezaji, ufuatiliaji, tathmini na utoaji wa taarifa. Hivyo, Maafisa Masuuliwanaelekezwa kuzingatia kikamilifu maelekezo yote yaliyopo kwenye Mwongozo wakati wa uandaaji, utekelezaji, na ufuatiliaji na tathmini ya mpango na bajeti. Miongoni mwa maelekezo hayo ni kama ifuatavyo:

 

3.2.1    Uandaaji

(i)          Kutenga bajeti kwa ajili ya shughuli za ushirikiano baina ya Serikali yaJamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar(SMZ);


(ii)        Kuandaa bajeti ambayo ni shirikishi kwa kuzingatia Muundo wa Mapato na Matumizi wa Muda wa Kati (MTEF) na ratiba iliyobainishwa kwenye Mwongozo;

 

(iii)      Kuimarisha Kamati za Bajeti na kuhakikisha kuwa Kamati hizo zinafanya kazi kwa mujibu wa Kifungu 18(2) cha Sheria ya Bajeti Sura 439;

 

(iv)      Kuhakikisha kuwa miradi inayoendelea kutekelezwa inatengewa fedha kwa ajiliya kuikamilisha kabla ya kuanza miradi mipya;

 

(v)        Halmashauri zenye mapato yasiyolindwa ya shilingi bilioni tano au zaidikutenga asilimia 60 kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo, ikijumuisha asilimia 10 kwa ajili ya Mikopo ya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu na asilimia 10 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya barabara zinazosimamiwa na TARURA;

 

(vi)      Halmashauri zenye mapato yasiyolindwa chini ya shilingi bilioni tano kutenga asilimia40 kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo ikijumuisha asilimia 10 kwa ajili ya Mikopo ya Wanawake, Vijana na Watu Wenye Ulemavu;

 

(vii)    Kupata idhini kutoka kwa Waziri mwenye dhamana ya masuala ya Fedha kabla ya kupokea mikopo, misaada na dhamana kwa mujibu wa kifungu cha 15(1) cha Sheria ya Mikopo, Dhamana na Misaada, Sura 134;

 

(viii)     Kuzingatia viwango vya ukomo wa bajeti vitakavyotolewa na Serikali;

 

(ix)      Kutumia Mfumo wa Kitaifa wa Kusimamia Miradi ya Maendeleo (NPMIS) katika kuandaana kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kuzingatia Waraka wa Hazina Na. 5 wa mwaka 2020/21;

 

(x)        Kuandaa na kuwasilisha mikakati ya uwekezaji ya taasisi, sera ya gawio (dividend policy) na mipango ya biashara katika Ofisi ya Msajili wa Hazinakwa ajili ya kupata idhini;

 

(xi)            Kukamilisha uhuishaji wa MipangoMikakati na wasifuwa taasisi ili iendane na vipaumbele vya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2021/22 – 2025/26); na


(xii)    Kuandaa bajeti ya maendeleo kwa kuzingatia vipaumbele vya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2021/22 – 2025/26).

 

3.2.2    Utekelezaji

(i)          Kuhakikisha mapato yote katika Wizara na Taasisi za Umma yanaendelea kukusanywa kupitia Mfumo wa Government e-Payment Gateway (GePG);

 

(ii)        Kuzingatia maelekezo ya Waraka wa Hazina Na. 2 wa Mwaka 2019 unaohusu utaratibuwa kuomba, kuhamisha, kupokea, kutumia, kuhasibu na kutoa taarifaza utekelezaji wa miradi ya D-Fund na matumizi ya Mfumo wa Usimamizi wa Fedha Zinazopelekwa Moja kwa Moja kwenye Miradi;

 

(iii)      Kuhakikisha ununuzi wa umma unafanyika kwa kuzingatia Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura 410 na Kanuni zake kwa kufanya ununuzi wa pamoja na kutumia Mwongozo wa Matumizi ya Force Account wa Mei 2020 ili kupata thamani halisi ya fedha;

 

(iv)      Kutumia Mfumo wa Kielektroniki wa Ununuzi wa Umma (TANePS) katika ununuzi wa bidhaa, huduma na kandarasi za ujenzi;

 

(v)        Kuendelea na utekelezaji wa Awamu ya Pili ya ujenzi wa Ofisi za Wizara katika Mji wa SerikaliMtumba Dodoma;

 

(vi)      Kuzingatia Sheria ya Msajiliwa Hazina, Sura 370 kwa kutenga na kuwasilisha katika Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikalimichango ya asilimia15 ya mapato ghafi ya Taasisina asilimia 70 ya ziada ya mapatobaada ya kutoa matumizi yaliyoidhinishwa;

 

(vii)    Kuzingatia Waraka wa Hazina Na. 7 wa Mwaka 2020/21 kuhusu utekelezaji wa miradi ya Ubia Baina ya Sekta za Umma na Binafsi (PPP); na

 

(viii)  Kuendelea kutekeleza Blueprint kwa kuboresha sheria mbalimbali ili kuweka misingimizuri ya kusimamiamazingira bora ya ufanyaji biasharana uwekezaji nchini.


3.2.3    Ufuatiliaji na Tathmini

(i)          Kuandaa mpango kazi na mtiririko wa fedha wa utekelezaji wa bajeti kupitia mifumo ya CBMS na PlanRep;

 

(ii)        Kuandaa taarifa za utekelezaji kwa kuzingatia muundo ulioainishwa katikaSura ya Pili ya Sehemu ya Pili ya Mwongozo.Taarifa za utekelezaji za kila robo ya mwaka ziwasilishwe katika muda wa siku 30 baada ya kukamilika kwa robo ya mwaka husika. Vilevile, taarifa za utekelezaji za mwaka ziwasilishwe kabla ya tarehe 15 Oktoba ya mwaka wa fedha unaofuata;

 

(iii)      Kujenga uwezo wa watumishi katika vitengo vya ufuatiliaji na tathmini na kuandaa mpango wa kurithisha watumishi wapya maarifa ili kuwa na mfumo endelevu wa ufuatiliaji;

(iv)      Kuendelea kutumia taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali katika kuboresha mifumo ya ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa mpango na bajeti; na

 

(v)        Kuongeza matumizi ya TEHAMA katika shughuli za Serikali ili kuongeza ufanisi ikiwa ni pamoja na kujengauwezo wa wataalamwa ndani kwenyeeneo la usalama wa mifumo.

 

32.            Mheshimiwa Spika, maelezo ya kina kuhusu maelekezo mahsusi ya Mwongozo yanapatikana katika Sehemu ya Pili, Sura ya Kwanza na Sura ya Pili ya Kitabucha Mwongozo.

 

4.0 MAPENDEKEZO YA MPANGO WA MAENDELEO WA TAIFA WA MWAKA 2022/23

33.            Mheshimiwa Spika,Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2022/23ni wa pili katika utekelezaji Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano, 2021/22 – 2025/26, wenye dhima ya “Kujenga Uchumi Shindani na Viwanda kwa Maendeleo ya Watu”. Katika mwaka 2022/23, Maeneomahsusi ya kipaumbele ni:

 

(i)             Kuchochea Uchumi Shindani na Shirikishi. Eneo hili linajumuisha miradi ambayo itajikitakatika: kujenga jamii yenye uwezo wa kushindana kikanda na kimataifa; kuimarisha utulivu wa uchumi jumla; kuimarisha mazingiraya biashara na uwekezaji; kuimarisha Tafiti na


Maendeleo (R&D) pamoja na uhawilishaji wa teknolojia kutoka nje; na kuendeleza miundombinu na huduma katika maeneo ya reli, barabara, madaraja, usafiri   wa maji, usafiri wa anga, TEHAMA, nishati, bandari na viwanja vya ndege;

 

(ii)           Kuimarisha Uwezo wa Uzalishaji Viwandani na Utoaji Huduma: Eneo hili linajumuisha miradi ya viwanda inayolenga kuongeza thamani ya mazao ya kilimo, mifugo, uvuvi na madini pamoja na kuzalisha bidhaa zitakazotumia malighafi na rasilimali zinazopatikana kwa wingi nchini. Aidha, eneo hili linajumuisha miradi na programu zinazolenga kuboresha sektaya utalii, huduma za fedhana bima;

 

(iii)         Kukuza Biashara na Uwekezaji: Eneo hili linajumuisha programu zitakazoimarisha masoko ya ndani na kutumia fursa za masoko kikanda na kimataifa. Masoko yanayolengwa ni yale yatakayotoa fursa kwa bidhaa na huduma zinazozalishwa nchini ikiwemo bidhaa na huduma zitokanazo na kilimo, viwandana utalii. Aidha, Serikali itaendelea kutekeleza Mpango Kazi wa Kuboresha Mazingira ya Biashara (Blue Print);

 

(iv)         Kuchochea Maendeleo ya Watu: Eneo hili linajumuisha utekelezaji wa miradi inayolenga kuboresha maisha ya watu ikiwemo kuboresha elimu na mafunzo katika ngazi zote; afya na ustawi wa jamii; hifadhi ya jamii; sensa ya watu na makazi; huduma za maji na usafi wa mazingira hususan mradi mkubwa wa maji kutoka ziwa Victoriahadi jiji la Dodoma; mipango miji, nyumba na maendeleo ya makazi. Aidha, eneo hili linajumuisha kuimarisha mfumo wa sheria na taasisi za utoaji haki na usimamizi wa utawala bora,ulinzi na usalama na utulivu wa ndani na nje ya nchi, mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi ikiwemo kuimarisha utoaji haki pamoja na ukuzaji wa maadili. Vilevile, Serikali itaendelea na utekelezaji wa shughuli za kuhamishia makao makuu ya Serikali Jijini Dodoma ikiwemo awamu ya pili ya ujenzi wa ofisi na miundombinu katika mji wa Serikali Mtumba; na

 

(v)           Kuendeleza Rasilimali Watu: Eneo hili linajumuisha programu na mikakati inayolenga kuendeleza ujuzi wa rasilimali watu nchini, kuanzia ngazi za elimu ya awali hadi elimu ya juu ikiwemo kuwawezesha vijana kujiajiri. Aidha, Serikali itaendelea kutekeleza Programu ya Kukuza Ujuzi Nchini kwa kutoa mafunzo ya ujuzi na stadi za kazi kupitia Programuya


Uanagenzi kwa vijana, kutoa mafunzo, kurasimisha na kutoa vyeti kwa vijana waliopata ujuzi nje ya mfumo rasmi pamoja na kutoa mafunzo ya vitendo mahali pa kazi kwa wahitimu wa elimu ya juu. Vilevile, eneo hili linajumuisha hatua za kuboresha viwango vya utoaji wa elimu ya ufundi na mafunzoya ufundi stadi pamoja na ujuzi adimu kwa lengo la kuongeza tija na ushindaniwa wananchi katika kutumia rasilimali zilizopo nchini ili kuleta maendeleo.

 

34.            Mheshimiwa Spika, Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2022/23 utajumuisha miradi ya kielelezo inayoendelea ambayo utekelezaji wake unatarajiwa kuwa na matokeo mapana na ya haraka katika uchumi. Miradi hiyo ni: Ujenzi wa Reli ya Kati kwa Kiwango cha Kimataifa (Standard Gauge Railway - SGR); Mradi wa Kufua Umeme wa Maji wa Julius Nyerere – MW 2,115; Kuboresha Shirika la Ndege Tanzania (ATCL); Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima (Uganda) hadi Tanga (Tanzania); Mradi wa Kuchakata na Kusindika Gesi Asilia kuwa Kimiminika (LNG) – Lindi; Mradi wa Magadi Soda Engaruka; Mradi wa Makaa ya Mawe - Mchuchuma na Chuma – Liganga; Mradi wa Kufua Umeme wa Maji wa Ruhudji (MW 358) - Njombe; Mradi wa Kufua Umeme wa Maji wa Rumakali (MW 222) - Njombe; Ujenzi wa Madaraja Makubwa na Barabara za Juu za Daraja la Kigongo - Busisi (Mwanza) na Daraja la Jipya la Selander (Tanzanite - Dar es Salaam); Bandari ya Uvuvi (Kilwa) na Ununuzi wa Meli za Uvuvi; Shamba la Miwa na Kiwanda cha Sukari Mkulazi; Utafutajiwa Mafuta na Gesi katika Kitalu cha Eyasi Wembere;Utafutaji wa mafuta na gesi katika kitalu cha Mnazi Bay Kaskazini; Kanda Maalumu za Kiuchumi ikiwemo Eneo Maalumu la Kiuchumi Bagamoyo; Ujenzi wa reli ya Mtwara – Mbamba Bay na matawi yake ya Mchuchuma na Liganga kwa kiwango cha SGR; Mradi wa kutoa maji wa Ziwa Victoriahadi Dodoma; na Kuongeza Rasilimali Watu yenye Ujuzi Adimu na Maalumu (Ujuziwa Kati na Wabobezi) kwa maendeleo ya viwanda na ustawi wa jamii ikiwemo ujenzi wa shule 26za wasichana katika mikoa yote.

 

Katika Kujenga Uchumi Shindani na Viwanda kwa Maendeleo ya Watu, Taifa linahitaji ushirikiwa sekta binafsiyenye uwezo wa kuchangia katikautekelezaji wa Mpango. Kwa msingi huo, Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji kwa sekta binafsi kwa kufanyia kazi maoni na ushauri wa kukabiliana na changamoto za sekta binafsi katika utekelezaji wa Mpango na miradi ya maendeleo.


35.            Mheshimiwa Spika, Maelezo ya kina kuhusu Maeneo ya Kipaumbele kwa mwaka 2022/23 yapo katika Kitabu cha Mapendekezo ya Mpango (Sura ya Nne).

 

5.0 HITIMISHO

 

36.            Mheshimiwa Spika, Mapendekezo ya Mwongozo na Mpango yatawezesha Mafungu kuandaa Mipangona Bajeti kwa Mwaka 2022/23.Kutokana na Mapendekezo haya, Maafisa Masuuliwa Wizara, IdaraZinazojitegemea, Wakala za Serikali, Sekretarieti za Mikoa, Mamlakaza Serikali za Mitaa, Taasisi na Mashirika ya Umma wanaelekezwa kuzingatiakikamilifu maelekezo yote yaliyopo kwenye Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali na Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka 2022/23. Aidha, wanaelekezwa kuzingatia kikamilifu Sheria ya Bajeti, Sura 439 na Kanuni zake.

 

37.            Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo naomba sasa Bunge lakoTukufu lipokee na kujadili Mapendekezo ya Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka 2022/23.

 

38.            Mheshimiwa Spika,naomba kutoahoja.