Familia moja katika eneo la Mumias, Kaunti ya Kakamega nchini Kenya imelazimika kulala nje ikipigwa na baridi baada ya Mama mwenye nyumba wao kuichoma nyumba yake moto kutokana na Wapangaji wake hao kutolipa kodi kwa wakati .
Taarifa iliyotolewa na DCI wa Kenya inasema Mama Mwenye nyumba anayeitwa Caroline Mukolwe alimfuata Mpangaji wake Teresia Ayeng Jioni ya juzi Alhamisi na kumtaka amlipe kiasi cha kodi anachomdai ambacho ni Ksh. 800 ( 16,494) lakini Teresia akalipa Ksh. 400 ( Tsh. 8,247), kupunguza deni huku akiahidi atalipa nyingine baadaye.
"Mama mwenye nyumba alipoona fedha ya kodi anayodai haijalipwa yote akarudi kwenye nyumba yake na kubeba mafuta ya taa akamwagia ndani ya nyumba kisha akaifunga na kuipiga kibiriti, Mpangaji akashuhudia mali zake zote zikiteketea kwa moto"DCI
Mama mwenye nyumba kwa sasa anashikiliwa na Polisi kwa kumsababishia hasara Mpangaji wake ya kuchoma mali zinazokadiriwa kuwa na thamani ya Ksh. 47,000 ( Tsh. Laki 9.69).