Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru aliyekuwa mhasibu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Godfrey Gugai na wenzake wawili baada ya mahakama hiyo kushindwa kuthibitisha mashtaka yaliyokuwa yakiwakabili.

Gugai na wenzake walikuwa wanakabiliwa na makosa 40, makosa 19 kati ya hayo ni kughushi, 20 ni utakatishaji fedha na moja ni kumiliki mali zilizozidi kipato halali.

Gugai alikuwa anakabiliwa na kosa la kumiliki mali kinyume na kipato chake, ambapo anadaiwa kutenda kosa hilo kati ya Januari 2005 na Desemba 2015.