Moja ya story kubwa wiki hii ni hii ya Kampuni ya Yahoo kufunga huduma zake nchini China huku ikitaja sababu kuwa ni kuongezeka kwa changamoto za kibiashara na mazingira halali ya kufanya shughuli zake, Yahoo iliingia China Mwaka 1999.

Yahoo inakuwa Kampuni ya Marekani ambayo inafunga huduma China siku za hivi karibuni, Google pia ilifunga huduma zake miaka kadhaa iliyopita na Mtandao wa Linkedln umesema utafunga pia huduma zake China.

China imeendelea kuipa nguvu mitandao yake yenyewe licha ya Kampuni kubwa kuondoka nchini humo, Baidu imekuwa search engine yenye nguvu China ikiwa ni mbadala wa Yahoo na Google huku WeChat na Weibo ikiwa ni mitandao inayofanya vizuri China.