Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi imekubali pingamizi la mawakili wa Serikali la kutopokea barua kama kielelezo cha ushahidi wa upande wa utetezi katika kesi ndogo ndani ya kesi kubwa ya ugaidi inayomkabili Mwenyeki wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu.

Uamuzi huo umetolewa leo Jumatatu Novemba 29, 2021 na Jaji Joachim Tiganga na kueleza kuwa mshtakiwa huyo Mohamed Ling'wenya hajaweza kuieleza mahakama ni kwa nini barua hiyo inamhuri wa naibu msajili.

Barua hiyo ni ile ya mshtakiwa wa tatu, Mohammed Abdillah Ling’wenya, kwenda kwa Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa Kipolisi Ilala (RPC), Dar es Salaam, ili kumuomba baadhi ya nyaraka alizitumie kwenye kesi yake ndogo.
 

Nyaraka hizo alitaka kuzitumia kuthibitisha na au kutothibitisha, kama askari polisi, Ricardo Msemwa alikuwepo katika chumba cha mashtaka cha Kituo Kikuu cha Polisi Dar ea Salaam, tarehe 7 Agosti 2020.

Akitoa uamuzi huo mdogo ya pingamizi la jamhuri dhidi ya barua hiyo, Jaji Tiganga amesema, mahakama imekataa kupokea barua hiyo kwa kuwa shahidi aliyeomba kuitoa hakujenga msingi wa mnyororo wa utunzwaji kielezo hiko hadi kumfikia (Chain of Custody).

Jaji Tiganga amesema, Ling’wenya alishindwa kuieleza mahakama hiyo namna barua hiyo ilivyotoka kwa naibu msajili wa mahakama hiyo kwenda kwake.

“Ni wazi sio nakala yake yeye, sababalu nakala yake yeye isingekuwa na mhuri wa naibu msajili, haya yangeweza kuthibitika kama angezungumza, angeweza kutumia nakala yake iliyotumika kum-save msajili.”

“Amekuwa mchumi wa maneno hajaeleza kwa nini barua inamhuri wa mahakama hivyo mahakama inabaki inajiuliza kilelezo anachotaka kukitoa kinafanana na kile kilichopelekwa kwa RPC Ilala. Mahakama haina majibu,” amesema

“Mahaka inaona kielelezo kilichopelekwa kwa RPC Ilala hatuwezi sema kama kinafanana na kilichopokelewa na RPC Ilala, shahidi ameshindwa ku-establish chain of custody.”

“Kwa kushindwa kutoa maelozo kwa nini kina mhuri na kama uligongwa na msajili ilikuwaje na kwa nini kilimrudia yeye. Ilikuwaje yeye hajataka kutoa kielelezo chake yeye na ku-tender kielezo cha mahakama. Shahidi ameshindwa kuthibitisha chain of custordy kwa sababu hiyo mahakama inakikataa kielezo hicho,” amesema Jaji Tiganga.