Mnamo Novemba mwaka huu kampuni ya simu Infinix ilizindua rasmi Infinix NOTE 11 na NOTE 11 pro. NOTE 11 series zimetushtua wengi kutokana na mabadiliko yaliyopo ambayo hayajawai kuwepo kwenye series za Infinix NOTE. Infinix NOTE 11 ina wigo mpana wa kioo cha inch 6.7fhd+ na inakuwa simu ya kwanza kwa series ya NOTE kuja na kioo aina ya AMOLED Display.  
 

Tufahamu kwanza Maana Ya AMOLED Display kabla sijakupa sababu za wewe kuvutiwa na simu hii ya Infinix NOTE 11.
 

AMOLED Display ni kioo ambacho kinaonesha picha kwa kwaliti kubwa sana na pia kina rangi ang'avu na halisia na zaidi ina ufanisi waharaka zaidi kuliko maoneshi mengine yoyote ya vioo, vioo hivi pia vinapunguza unyonyaji wa chaji yaani ukiwa na amoled display kwenye simu yako au kwenye tv yako basi matumizi ya beteri huwa madogo zaidi.
 


FAIDA ZA AMOLED DISPLAY

1.Hutumia Chaji kwa udogo zaidi.
kulingana na sifa ya kioo iki mtumiaji wa Infinix NOTE 11 anafaidika mara mbili zaidi kwenye swala uhimara wa simu kudumu na chaji japokuwa tayari kioo chenye sifa yake kuu ni kutunza chaji lakini pia ni simu yenye battery la ujazo mkubwa wa mAh 5000 hivyo mtumiaji anaweza maliza siku mbili na zaidi pasipokuichaji na bado anaendelea kufurahia huduma zitokanazo na simu yake.
 
2. Hutumia Nguvu Ndogo.
Likija kwenye swala la kuperuzi ni sawa na kuteleza tu haina haja ya kutumia nguvu  sababu ni kioo chenye layers chache na zenye uhimara na kuweza kusense vidole vya binadamu kwa haraka sana.
 
3. Huzipa picha rangi halisi
Mtumiaji wa NOTE 11 pamoja ya kuwa simu yake ina camera ya Megapixel 50 yeny e kutumia teknolojia ya AI lakini pia anafaidika na kioo hiki kutokana na yakuwa ni kioo kilichojazwa uwezo wa kubalance rangi ya picha. Kwa pamoja teknolojia ya AI na AMOLED vinafanya kazi sambamba kupiga picha zenye rangi halisi.  
 
4. Mvuto wa umbo la simu
kila mtu anapenda kitu chenye kuvutia, kutokana na AMOLED Display umbo la simu hii ni jembamba na lenye kuvutia, ni simu yenye kutia hamasa kuwa nayo hata kabla ya kufahamu kilicho ndani unaweza kuihadhi popote iwe kwenye wallet, mfuko wa suruali au sharti pasipo wadukuzi kukugundua.
 
FEATURES NYENGINE ZA INFINIX NOTE 11.
1. Kulingana kwa ubora kati ya picha ya mbali na karibu.
Sifa nyengine ya Infinix ni namna teknolojia ya kuzoom inavyoweza kuvuta picha mara 30X na bado picha ikaonekaonekana na mvuto sawa na ile iyochukuliwa pasipo kuzoom.
 

2. Kujaa kwa chaji kwa haraka.
Infinix NOTE 11 inatumia mfumo wa fast chaji wenye Wh33 uhakika wa kujaza battery kwa lisaa limoja lakini pia kulingana na ujazo wa battery Infinix NOTE 11 inadumu na chaji kwa muda mrefu.
3. Kutunza kumbukumbu kwa usalama zaidi.
Infinix NOTE 11 ni simu yenye bei rafiki lakini ni simu yenye storage kubwa ya GB 128 hata pasipo memory ya Zaida bado unauhakika wa kuhifadhi vitu vyako vingi na kwa usalama zaidi kwani tunafahamu chanzao cha kuweka memory card zisizothibitishwa huleta wadudu kwenye simu zetu.
 
Infinix NOTE 11 inapatika katika rangi tatu tofauti nyeupe, green na nyeusi https://www.infinixmobility.com/