Sera za matangazo ya Facebook, Instagram, Twitter ni mwongozo unaotumika na mtandao huo wa kijamii kusimamia matangazo yanayotengenezwa na watumiaji wake.
Facebook, instagram na Twiiter hutumia sera hizi kupitia tangazo na kuhakiki kama vigezo na masharti yao ya matangazo yamezingatiwa.
Wafanyabiashara na watu binafsi wamekuwa wakitangaza bidhaa na huduma zao kupitia mtandao huu wa kijamii na hii imepelekea wao kufanya mauzo hata kwa watu walio mbali na ofisi zao.
Sera za matangazo ya Facebook, Instagram, Twitter zinazotumika kama muongozo kwa watumiaji wa huduma hii ni.
1. Mchakato wa Kukagua Matangazo:
Matangazo yote kabla ya kuchapishwa na kuwa hewani ni lazima yapitie ukaguzi utakaobaini kama vigezo na masharti yaliyopo kweye sera ya matangazo ya mtandao husika vimezingatiwa.
Katika ukaguzi hupitia maneno, picha na video inayotumika kwenye tangazo lako kisha kulichapisha kama hakutakuwa na uvunjifu wa sera, pia tangazo linaweza kukaguliwa tena hata likiwa hewani.
2. Nini cha kufanya ikiwa tangazo lako limekataliwa?
Tangazo lako linapokataliwa baada ya ukaguzi unaweza kulibadilisha, kuomba likaguliwe upya kama unahisi halina shida yoyote au kuandika upya Tangazo lingine.
3. Maudhui Yaliyokatazwa:
Maudhui yaliyokatazwa ni pamoja na kuwezesha, au kutangaza bidhaa, huduma au shughuli haramu, Matangazo yanayohusu ubaguzi wa aina yoyote, Tumbaku na matumizi yake, Madawa ya kulevya, Silaha na matumizi yake, Maudhui ya Kusisimua, Ukiukwaji wa hati miliki, Sifa za mtu binafsi kama dini, Habari potofu, Maudhui yenye utata, Udanganyifu na Matendo ya Udanganyifu na Uuzaji wa Viungo vya Mwili.
4. Maudhui Yaliyozuiwa:
Kuna baadhi ya maudhui ambayo yamezuiwa kulingana na vigezo vya ziada ambavyo huhitajika ili uweze kuchapisha tangazo la aina hiyo. Matangazo yaliyozuiwa ni pamoja na Matangazo ya pombe, Matangazo ya Kamari, Utangazaji wa Dawa za Kulevya, Huduma za Usajili na Maudhui yenye Chapa.
5. Matangazo ya Video:
Katika upande wa video matangazo ya facebook hayaruhusu video zenye maudhui yanayovuruga au yenye vurugu, pombe na madawa ya kulevya na Lugha chafu.
6. Uchaguzi wa Walengwa:
Kwasababu mitandao ya kijamii inamruhusu mtumiaji wa huduma yake ya matangazo kuchagua ni aina gani ya watu yanayowalenga imeweka pia na kizuizi kuhakikisha kuwa watu hawatumii vibaya fursa hii kunyanyasa, kubagua, kuchokoza na kuwadharau watumiaji wengine kupitia matangazo hayo.
7. Uwekaji wa Matangazo:
Unapoandaa tangazo lako unatakiwa kuhakikisha kuwa maneno uliyoyaandika katika tangazo lako yanaendana na bidhaa au huduma inayoonekana kwenye picha utakayotumia. Pia hairuhusiwi kuambatanisha tangazo lako na tovuti yenye maudhui yaliyokatazwa katika sera zingine.