Na WAMJW- Mwanza

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima amefanya ziara ya kukagua Maendeleo ya jengo la mama na mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza- Sekou-Toure.

Katika ziara hiyo ameagiza kasi iendelee katika kukamilisha mradi huo ambao sasa uko asilimia 88 na huduma za uzazi zianze kutolewa katika jengo hilo kabla ya Januari, 2022 kama Mkandarasi alivyoahidi.

Dkt. Gwajima ameelekeza kuanzishwe daftari la kuandika taarifa ya kilichotekelezwa Kila siku ili kuweza kuongeza kasi na kujua kila hatua katika mradi huo ili kuongeza uwajibikaji.

Katika ziara hiyo Dkt. Gwajima aliambatana na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Dkt. Thomas Lutachunzibwa.