Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amesema zoezi la kuwapanga vizuri Wamachinga katika Jiji la Dar es salaam limeenda salama pasipo usumbufu wowote na kusema kwa sasa ameagiza maeneo walipoondoka Machinga yasafishwe na yafanyiwe ukarabati.

"Maelekezo ya Rais samia yalikuwa zoezi lifanyike pasipo matumizi makubwa ya nguvu wala kudhalilisha Mtu, nashukuru maeneo yote mambo yameenda Vizuri" RC Makalla

Makalla amesema zoezi la kuwapanga Vizuri Machinga limekamilika na sasa hatua inayofuata ni usafi wa hali ya juu Dar es salaam ——— "Kikwazo cha usafi DSM ilikuwa biashara holela, nashukuru hili tumelikwamua, tujiandae kwa usafi endelevu"