Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara ndugu Philip Japhet Mangula  Novemba 03 amefungua Mafunzo ya Makatibu wa Mikoa Na Wilaya Nchi Nzima katika ukumbi wa H/KUU Makao Makuu ya CCM jijini Dodoma.

Pamoja na Mambo mengine ya msingi lengo la mafunzo hayo ni kujenga uelewa juu maadhumuni na Imani ya CCM sanjali na mambo mbalimbali ya ujenzi wa Taifa letu.

Aidha Mafunzo hayo yatafanyika kwa siku tatu na zaidi ya mada 17 zitafundishwa na wakufunzi mbalimbali waandamizi wa Chama na Serikali.

Mafunzo hayo yatahitimishwa tarehe 6 Novemba, 2021 ambapo Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufunga Mafunzo Hayo.