Club ya FC Barcelona imemtangaza kiungo na nahodha wao wa zamani Xavi Hernandez kuwa kocha wao mpya kwa mkataba wa miaka mitatu utakaomuweka Nou Camp hadi 2024.

Xavi ameanzia soka la vijana katika kikosi cha FC Barcelona 1991, baadaye 1998 akapanda timu ya wakubwa hadi alipoondoka 2015 na kujiunga na Al Sadd ya Qatar kama mchezaji (2015-2019) na akaanza kazi ya ukocha akiwa na kikosi hicho 2019-2021.