Daktari wa mifugo wa kijiji cha Loiborsoit A wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara, Malipe Ole Kisota ameuawa kwa kukatwa mapanga na watu waliomtuhumu kumpa miamba mke wa ndugu yao.

Imeelezwa kuwa alikatwa na sime sehemu mbalimbali mwilini na ndugu watatu, Lazaro,  Mamei na Supek Mamei, wakimtuhumu kumpa ujauzito mke wa ndugu yao Kinaruu Mamei.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Manyara, Marrison Mwakyoma akizungumza Novemba 13,2021 amesema kuwa mauaji hayo yametokea Novemba 11,2021.

Kamanda Mwakyoma amesema chanzo cha kifo hicho ni wivu wa mapenzi, akidai marehemu alikuwa akituhumiwa kutembea na mke wa mtu na alikuwa anatafutwa akawa anajificha na siku ya tukio walimkibiza, kumkamata na kufanya mauaji hayo.

Kamanda Mwakyoma amesema watuhumiwa hao watatu walitoroka kusikojulikana mara baada ya mauaji hayo ila wanaendelea kuwatafuta ili wawafikishe mahakamani.

Credit: Mwananchi