Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma linamshikilia Mwanaume mwenye miaka 25 Mkazi wa Ilazo kwa tuhuma za kumbaka Mwanamke mjamzito mwenye miaka 23 na kumsababishia maumivu makali, huku chanzo cha tukio hilo kikisemekana kuwa ni tamaa za kimwili.

Taarifa hizo zimetolewa jana Novemba 22, 2021 na Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma Onesmo Lyanga ambapo amesema mtuhumiwa huyo alimvamia mwanamke huyo akiwa amelala na kutekeleza tukio hilo.

"Alimbaka mama mjamzito kwa visingizio mbalimbali aidha vya ulevi, sijui nilipotea mlango lakini suala ni kwamba kosa la ubakaji limefanyika, yeye aendelee kutoa utetezi wake lakini sisi tunachukua sheria muda si mrefu atafikishwa katika vyombo vya sheria" alisema Kamanda huyo wa Polisi.