Waziri wa Afya wa Afrika Kusini ametoa wito wa kile alichokita kuondolewa kwa marafuku ya kusafiri ya kibaguzi ilizowekwa dhidi ya mataifa ya kusini mwa Afrika kutokana na kuzuka kwa aina mpya kirusi ya Omicron.
Katika hotuba yake kwa shirika la afya duniani WHO, aliyoiwasilisha nchini Uswisi, Joe Phaahla amesema anahisi hiyo hatua ni ya kibaguzi kwa kuwa marufuku hiyo haijawekwa katika matraifa mengine ambayio kirusi hicho kimegundulika.
Nae Waziri wa Afya na Huduma za Kibinadamu wa Marekani, Xavier Becerra, aliuambia mkutano huo wa WHO kwamba wanafanya kazi kwa pamoja na mwenziwe wa Afrika Kusini ili kufahamu zaidi kuhusu aina hiyo ya kirusi na kuhamasisha namna ya kukidhibiti.