Mitandao mbalimbali imeeipoti kwamba Mwimbaji staa wa Uingereza Adele kwa hasira aliamua kuvunja mahojiano yake na Mtangazaji wa Australia Matt Doran na kutoka nje baada ya Mtangazaji huyo wa TV kusema hajaisikiliza album mpya ya Adele "30".

Pamoja na Mtangazaji huyo kusafiri maili 10,000 kutoka Sydney Australia hadi London kwa sababu tu ya kumuhoji Adele, alikatazwa asirushe kokote Interview hiyo kutokana na kitendo hicho, ilikuwa ni Adele wakati anakaa kwa ajili ya Interview alimuuliza Mtangazaji huyo wa "Weekend Sunrise" anafikiria nini kuhusu album yake mpya "30" ambapo Jamaa alikiri "sijaisikiliza", Adele akatoka nje kwa hasira huku lebo yake ya Sony ikakataza Interview hiyo kutotumika sehemu yoyote.

Baadae Mtangazaji huyo aliliambia Gazeti la The Australian kwamba amesikitishwa na anaomba msamaha kwa Adele huku akisisitiza kuwa lilikuwa ni kosa la kawaida tu "Wakati najiandaa kufanya Interview sikujua kabisa kwamba nilikuwa nimetumiwa email yenye hakikisho la albamu yake ambayo ilikua haijatolewa, hata hivyo nasisitiza Adele hakutoka nje"