Abu Dhabi wamezindua Taxi isiyoendeshwa na Dereva (Driverless Taxi) ambayo imepewa jina la Txai ambapo sasa kinachosubiriwa ni majaribio yake mwishoni mwa mwezi huu kwenye kisiwa cha Yas ambapo Serikali ya Abu Dhabi imesaini makubaliano ya kushirikiana na Bayanat ambayo ni Kampuni inayohusika na magari haya.

Taxi hizi zisizo na Dereva zitafanya kazi ya kubeba abiria yeyote bila malipo katika maeneo ya Kisiwa cha Yas cha Abu Dhabi ambapo kuna APP maalum ambayo Watu watatakiwa kuwa nayo kwenye simu ili kubebwa bure kwenye taxi hizi.


Magari matatu kati ya haya yatayohusika kwenye majaribio ni ya umeme na mawili ni ya mafuta kawaida, juu ya magari hayo kuna sensa, camera na teknolojia inayoliwezesha kujiendesha lenyewe bila kukosea chochote barabarani.