NA OSCAR ASSENGA,TANGA
WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa ameitaka Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kuhakikisha inaangalia kitengo cha mauzo kwa sababu hakijakaa vizuri huku  akiwataka wafanye mabadiliko makubwa kwa kuwa na watu wenye mtazamo mkubwa wa kutafuta biashara na sio wa kukaa ofisini na kupiga maneno.

Aliyasema hayo wakati wa ziara yake kutembelea ukarabati wa Bandari ya Tanga ambapo alisema atafanya mabadiliko katika maeneo hayo kwa sababu Serikali inawekeza fedha nyingi hivyo bila kuchangamka bila kwenda mbali kupambana kutafuta wateja hawatapata.
 

Alisema kwa sababu duniani kuna ushindani mkubwa huku akiielekeza TPA kwenye kitengo cha Mauzo na Baishara lazima wabadilike waweke watu wazuri ambao wanaweza kuuza Bandari ya Dar ,Tanga na zote za Tanzania .


“Hili tumeliona tutafanya mabadilko makubwa wala sio natania kuhakikisha kila mteja anakuja anahudumiwa kama mfalme sio anakuja mteja anasema maneno anapuuzwa tu hii haipo sawa na hatutakubali kuona hili linaendelea”Alisema 

Hata hivyo alisisitiza kuwa miradi yote ya ujenzi na upanuzi wa bandari za Tanga, Dar na Mtwara lazima zisimamiwe na wahandisi washauri ambao watahakikisha kazi ziko katika viwango vya ubora na kuweka juhudi kubwa katika mikakati ya uuzaji kwa kuweka wataalam kwenye hati hiyo.

Kwa upande wa teknolojia mpya ya mita za mtiririko wa mafuta 'Corlious Mass Flow' iliyowekwa kwenye bandari tatu za Tanga, Dar es Salaam na Mtwara imefanikiwa kuondoa wizi wa mafuta kwa sababu ina uwezo wa kufanya kazi sita za kupima joto, shinikizo, wiani, misa, ujazo, mnato na umakini mara moja kwa hivyo kuamuru ripoti zote za rekodi za mita za mtiririko zinapaswa kukusanywa na kuratibiwa katika kituo kimoja cha uti wa mgongo cha Dar es Salaam chenye lengo la kuzidhibiti.

Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga Donald Ngaile ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eric Hamisi amesema urekebishaji wa mita mpya ya teknolojia, Kituo cha Mafuta cha Tanga kimeongeza idadi ya meli za mafuta ambazo zinashusha shehena ya mafuta hadi matangi tisa kwa mwezi na sita ya mafuta.

Ambapo alisema shehena ya mafuta kwenye visiwa vya Zanzibar na ina uwezo wa kupima lita 1200 kwa saa na kutoka Februari bandari iliweza kuhudumia shehena ya mafuta kwa wateja kutoka Rwanda, Kenya Uganda, Msumbiji, Kongo na Zambia.

Alisema ujenzi wa ukarabati huo hivi sasa umefikia asilimia 14.5 na utakapokamilika wanatarajia kuwepo ongezeko la shehena mara nne ya kiwango kinachohudumiwa sasa na uwezo wa Bandari iliyopo sasa ni tani 750,000 na ujenzi ukapokamilika itafikia tani milioni 3 kwa mwaka na wataanza kuhudumiwa shenena kutoka Kigali nchini Rwanda  na nyengine ambazo hazipiti hapo.