Watu tisa wamefariki dunia na wengine wamejeruhiwa baada ya basi  la Emigrace linalofanya safari zake kati ya Babati Mkoa wa Manyara na Dar es Salaam kupinduka.

Ajali hiyo imetokea leo Jumamosi Oktoba 2, 2021  katika mteremko wa milima ya Kolo Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Besta Magoma amesema miili ya watu hao imehifadhiwa Hospitali ya Wilaya ya Kondoa.