Nchini Norway, mtu aliyekuwa amejihami kwa mishale amewashambulia na kuwauwa watu watano na kuwajeruhi wengine wawili katika mji wa Kongsberg, Kusini Magharibi mwa nchi hiyo. Mmoja wa waliojeruhiwa ni afisa wa polisi.

Polisi wanasema, mshukiwa,  mwenye umri wa miaka  37, amekamatwa, lakini lengo la shambulizi hilo halijabainika.

Ripoti zaidi zinasema, mshukiwa huyo alikuwa anatembea kwenye mji wa Kongsberg, akiwashambulia watu.

Mshambuliaji anasemekana kufanya tukio hilo ndani ya duka la jumla la Coop Extra iliopo upande wa Kongsberg magharibu.

Polisi wanaamini alitekeleza shambulio hilo peke yake, na watachunguza ikiwa ni kitendo cha ugaidi.

-RFI