Kongamano la Umoja wa Mataifa la Mabadiliko ya Tabianchi (COP26) limeanza leo katika mji wa Glasgow nchini Scotland huku kukiwa na indhari ya jamii ya wanasayanbsi kuwa sayari ya dunia inakabiliwa na hatari kubwa kutokana na mabadiliko ya tabia nchi.

Wawakilishi  wa nchi 200 Ulimwenguni kote wanatazamiwa kutoa maamuzi muhimu ya pamoja mpango wa 2030 wa kuzuia majanga ya tabia nchi.

Kutokana na ongezeko la joto duniani na shughuli za uuzaji wa mafuta, wanasayansi wanaonya kwamba hatua za haraka zinahitajika ili kuepuka janga la mabadiliko ya tabia ya nchi.

Katika ufunguzi wa kikao hicho,  taarifa ya ripoti ya mabadiliko ya tabia nchi iliyotolewa na Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) itawasilishwa kwa washiriki.

Ripoti ya WMO ya wanasayansi wa hali ya hewa italinganisha viwango vya joto duniani mwaka huu na miaka iliyopita.

Matukio makubwa ya hali ya hewa yanayohusishwa na mabadiliko ya tabia nchi - ikiwa ni pamoja na mawimbi ya joto, mafuriko na moto unaoukumba misitu kuongezeka.

Rekodi zimeonyesha kuwa muongo uliopita ulikuwa wa joto zaidi jambo lililohitaji zaidi hatua za haraka na pamoja. Mkutano wa Umoja wa Mataifa ni moja ya mikutano mikubwa zaidi ambayo Uingereza imewahi kuandaa, na ilicheleweshwa kwa mwaka mmoja kwa sababu ya janga hilo. COP inasimamia 'mkutano wa nchi wanachama' na ni mkutano wa 26.

Hivi karibuni, Mkuu wa shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO na mashirika mengine tisa ya kimataifa yametoa wito wa pamoja na wa dharura kwa serikali kuweka kipaumbele kwa hatua jumuishi za maji na mabadiliko ya tabianchi kutokana na athari zinazoenea za masuala hayo kwa maendeleo endelevu.