Vyombo vya habari vya serikali ya Korea Kaskazini vimeonyesha picha za video za wanajeshi wakionyesha uwezo wao wa kupigana na uwezo wa kuvunja vitu mbali mbali kwa mikono yao .

Onyesho hilo la warsha ya ulinzi huko Pyongyang, na lilitazamwa na viongozi pamoja na Kim Jong-un.

Licha ya kuharibu matofali na vigae, askari walionekana wakiwa wamelala juu ya vitanda vya vioo na misumari.

Kilele cha maonyesho kilihusisha wanaume wakikunja chuma kutumia shingo zao na kuvunja minyororo.

Vyombo vya habari vya Korea Kaskazini vilisema ni kuonyesha maadui kwamba wanajeshi wao walikuwa na "ngumi za chuma kulinda amani ya nchi".

 

Credit:BBC