Utafiti uliofanyika unaonyesha asilimia kubwa ya kundi linaloumizwa kwenye mapenzi ni upande wa mwanamke.Kutokana na kuumizwa huko zipo sababu nyingi sana ila kati ya sababu hizo nyingi zinachangiwa na upande huo wa kike na kupelekea hali hiyo.

Leo hii nimekuandalia mambo muhimu manne ambayo wanaume hawayapendi kutoka kwa wapenzi wao na wengi wao huwa hawayasemi, wanaamua kuchukua maamuzi ambayo sio sahihi ya kuachana na mwanamke wake.


1.Wivu wa kupindukia
Mwanamke mwenye wivu wa kupindukia humfanya mwanaume kukosa amani kwani hata awapo kazini kwake mwanamke atataka kumfuatilia na kumnyima uhuru.

Hawa wenye tatizo hili huachwa na wanaume wao haraka kwani wengi hawapendi kuonewa wivu wa hivyo, wengine huuita wivu wa kijinga.

2.Kujipamba kupitiliza
Mwanamke kama mwanamke ni mapambo na ili awe mwanamke anao ulazima wa kuhakikisha anaonekana smati kwa kujipamba lakini si kama wafanyavyo wanawake wa siku hizi.

Wanaume wengi wamejikuta wanachukizwa na hali ya mwanamke kujipamba kupitiliza.

Yaani unakuta mwanamke anajipamba utadhani siku hiyo ni siku yake ya kufunga ndoa, hilo ni tatizo na husababisha hata mwanaume kuogopa kuongozana naye.

Sasa je, kama unatoka na mume au mpenzi wako, unajipamba hivyo kumfurahisha nani hasa? Mbona ukiwa nyumbani unakuwa wa kawaida tu?

3.Matumizi makubwa ya fedha
Mwanamke mwenye matumizi makubwa ya fedha ambaye hafikirii kesho itakuwaje ni adui mkubwa wa mwanaume.

Hata kama atakuwa anakupenda kiasi gani, atakuvumilia siku za mwanzo lakini kadiri mnavyokwenda atajitoa kwako taratibu. Hii ni kwa sababu mwanaume atahisi siku akija kuwa hana kitu anaweza kuibiwa na wenye fedha.

4.Muongeaji sana
Mwanamke muongeaji sana asiyekuwa na staha, mwanamke ambaye hawezi kumvumilia mwanaume pale anapokuwa akimsema kwa jambo f’lani kwa nia ya kutaka maelewano ni tatizo.

Namzungumzia yule ambaye muda wote anataka kushindana na mume/ mpenzi wake katika kuongea, yaani kuonesha kuwa hajakosea, anaonewa au na yeye yumo kwenye kuongea, huyu hawezi kumshika mtu wake.

Mwanamke anayeijenga ndoa yake anatakiwa kuwa chini pale mwanaume anapokuwa anapaza sauti, akishapoa na wote mmepoa. kama una dukuduku lako ongea naye taratibu.

Haiwezekani mume na mke kuwa juu hasa mnapokuwa kwenye mgogoro, inatakiwa mwanamke kumsoma mume wake au mpenzi wake kwa wakati huo.