Kamanda wa vikosi vya ardhi nchini Uganda, Jenerali Muhoozi Kainerugaba, ameweka kwenye Twitter picha ya kile anachosema kuwa gari la kwanza la kivita kutengenezwa nchini humo.

Anasema "liliundwa na kutengenezwa ncini Uganda", lakini hakutoa maelezo kuhusu muundo na gharama yake.

Gari hilo lililopewa jina la Chui - lilizinduliwa na  Rais Yoweri Museveni.