Serikali imepokea shehena ya dozi  1,065,000 za chanjo ya UVIKO-19 aina ya Sinopharm huku ikiweka wazi baada ya uhakiki wa kimaabara itasambazwa nchi nzima ili kuongeza kasi ya uchanjaji ikiwa ni jitihada za kukabiliana na ugonjwa huo.

Akizungumza mara baada ya kupokea shehena hiyo ya Chanjo Waziri wa Afya Dkt.Doroth Gwajima amesema ujio wa chanjo hiyo unawapa fursa wananchi kuchagua chanjo ambayo wanayotaka ambazo ni salama na uliokubalika kisayansi.

“Mpaka sasa wananchi waliochanjwa chanjo ya UVIKO-19 wamefikia 760,962 sawa na asilimia 74.4% kwa Tanzania bara na watu 10,800 Zanzibar na inaendelea kwa hiali bila malipo katika vituo vyote nchini”. Amesema Dkt.Gwajima.

Amesema Shirika la Afya Duniani (WHO) imethibitisha usalama wa chanjo hizo na kuzipitisha hivyo kuna wataalamu hapa nchini pia huzipitia kabla ya kuzipeleka kwa wananchi.

Amesema lengo la Serikali ni kufikia uchanjaji wa asilimia 60 ya watanzania kikubwa kufuata mwaongozo wa utoaji wa chanjo hizo na wizara hiyo.