Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Profesa Abel Makubi ametoa kauli hiyo wakati akizungumzia mkakati wa Serikali, taasisi na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali.
Profesa Makubi amesema lengo hilo wanajua litatimia kwa kuwa wameamua kuwa na watu ambao wanafanya kazi hadi ngazi ya chini kwa walenga hivyo elimu itafikishwa moja kwa moja.
Chanjo zinazolengwa ni dozi 1,065,000 za Sinopharm ambazo ziliingia nchini Oktoba 8,2021 katika mpango wa msaada wa Covax.
Kabla ya dozi hizo, tayari Tanzania ilishapokea dozi 1,058,400 za chanjo ya Johnson & Johnson ambazo Katibu amesema kuwa zilishaisha.