Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) anawatangazia Watanzania wenye sifa kuomba kuajiriwa katika nafasi za kazi zifuatazo:
1.1 AFISA UCHUNGUZI (NAFASI 200)
1.2 Sifa za Kitaaluma:
Muombaji awe angalau na elimu ya shahada ya kwanza iliyotolewa na chuo kinachotambulika na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika fani zozote kati ya hizi: Mambo ya Kale na Utalii, Sheria, Uhasibu,Teknolojia ya Habari, Elekitroniki, Misitu, Kilimo, Ununuzi, Uchumi na Mipango, Usimamizi wa Rasilimali Watu, Takwimu, Utawala wa Umma/Serikali, Utunzaji wa Kumbukumbu, Usimamizi na Uthamini wa Ardhi, Mafuta na Gesi,Ukadiriaji wa Majenzi, Uhandisi wa Umeme, Uhandisi katika Kemia, Mifugo, Usanifu wa Majengo, Mambo ya anga, Uhandisi wa Mitambo, Uhandisi wa Ujenzi na Uhandisi wa Maji;
2.1 MCHUNGUZI MSAIDIZI (NAFASI 150)
2.2 Sifa za Kitaaluma:
Muombaji awe na cheti cha elimu ya kidato cha nne (CSE) au kidato cha sita (ACSE). astashahada au stashahada ya fani yoyote inayotolewa na Taasisi au chuo kinachotambulika na Serikali ya Tanzania, pamoja na fani kama vile ujenzi, ulinzi, udereva, upakaji rangi, ufundi magari, vifaa vya muziki, utunzaji wa kumbukumbu , TEHAMA, maendeleo ya jamii, uhazili, menejimenti ya hotel , n .k.
Mwisho wa kutuma maombi ni - 8th November, 2021
👉Kujua zaidi pamoja na kutuma Maombi <<BOFYA HAPA>>
👉Kupata nafasi mbalimbali za kazi Serikalini na mashirika binafsi <<BOFYA HAPA>>