Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) inapenda kufahamisha umma na wadau wa Elimu ya Juu nchini kuwa Awamu ya Nne na ya mwisho ya Udahili kwa ngazi ya Shahada ya Kwanza katika Taasisi za Elimu ya Juu nchini kwa mwaka wa masomo 2021/2022 umekamilika.
 

WAOMBAJI WALIODAHILIWA KATIKA CHUO ZAIDI YA KIMOJA 

Waombaji waliodahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja katika Awamu ya Nne na wale ambao hawakuweza kuthibitisha udahili katika awamu zilizopita wanasisitizwa kuthibitisha udahili wao katika chuo kimojawapo kuanzia tarehe 24 Oktoba hadi 6 Novemba, 2021 kwa kutumia namba maalum ya siri iliyotumwa kwa ujumbe mfupi kupitia namba zao za simu au barua pepe walizotumia wakati wa kuomba udahili. 

Wale ambao hawatapata kwa wakati ujumbe huo, wanashauriwa kuingia kwenye mifumo ya udahili ya vyuo walivyodahiliwa na kuomba kutumiwa ujumbe mfupi wenye namba maalum ya siri iii kuweza kujithibitisha katika chuo husika. Aidha, uthibitisho wa udahili ufanyike kupitia akaunti ambayo muombaji alitumia wakati wa kuomba udahili.

Kuona Orodha ya majina ya waombaji waliodahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja katika Awamu ya Nne na wale ambao walishindwa kuthibitisha udahili katika awamu zilizopita imewekwa katika tovuti ya TCU  Bofya Hapo Chini.

 

<<BOFYA  HAPA KUTAZAMA MAJINA YOTE>>