Chuo Kikuu cha Dodoma kinapenda kutaarifu Umma kuwa mnamo tarehe 25 Oktoba, 2021 kilipokea kwa masikitiko makubwa taarifa za tuhuma dhidi ya Mtumishi wake ndugu Petro Bazil Mswahili ambaye ni Mwanataaluma juu ya kujihusisha na rushwa ya ngono kinyume na maadili ya Utumishi wa Umma. Baada ya kupokea taarifa hizo, Chuo kimeanzisha mchakato wa hatua za kinidhamu na maadili kulingana na Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma.
 

Aidha, Mtumishi huyu alisimamishwa kufanya majukumu yake yote yakiwemo kufundisha kuanzia tarehe 25 Oktoba, 2021 hadi uchunguzi utakapokamilika.
 

Chuo Kikuu cha Dodoma kimekuwa kikichukua hatua stahiki za kinidhamu kwa mujibu wa Sheria na Taratibu za Utumishi wa Umma bila kumuonea mtumishi yoyote.
 

Aidha, Chuo kinapenda kuutaarifu Umma kuwa kitendo hiki hakivumiliki wala kukubalika na kwamba wakati wote Chuo kitaendelea kusimamia nidhamu na maadili kwa watumishi wake wote. 

Pia, Chuo kitaendelea kuchukua hatua kali kwa mtumishi yeyote atakayebainika kujihusisha na makosa ya kinidhamu.
 

Chuo kimesikitishwa sana kwa usumbufu uliojitokeza.
 

IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA UHUSIANO KWA UMMA NA MASOKO
CHUO KIKUU CHA DODOMA