Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) Laongeza safari zake za ndani na nje ya nchi
Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) limeongeza safari zake za ndani na nje ya nchi, kuanzia mwezi Novemba mwaka huu.
Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa ATCL Josephat Kagirwa amesema safari zilizoongezwa ni pamoja na za Dodoma- Mwanza, Dar es Salaam – Mtwara, Dar es Salaam – Bujumbura, Dar es Salaam – Lubumbashi pamoja na Dar es Salaam – Nairobi.
Kagirwa amesema ongezeko la safari hizo ni linatokana na ujio wa ndege mbili hivi karibuni na ni utekelezaji wa mpango mkakati wa shirika hilo, ambapo lilijipanga kupanua safari zake kwa kuongeza ndege.
Akizungumzia ujio wa ndege hizo aina ya Airbus A220-300, Kagirwa amesema zitakuwa na uwezo wa kubeba abiria 132, na kati ya hao 12 wa daraja la biashara na 120 daraja la uchumi.