Bomu lililotegwa mlangoni mwa msikiti wa Eidgah mjini Kabul, limelipuka na kuwajeruhi watu kadhaa waliokuwa wanahudhuria ibada ya kumbukumbu ya mama wa msemaji wa Taliban Zabihullah Mujahid.
Hadi sasa hakuna kundi lililokiri kuhusika na shambulio hilo, Lakini Tangu Taliban ilipochukua udhibiti wa Afghanistan katikati ya mwezi Agosti, mashambulizi yanayofanywa na kundi linalojiita dola la kiislamu dhidi ya kundi hilo yameongezeka.
Hatua hiyo imeongeza hofu ya kutanuka mgogoro mkubwa zaidi kati ya makundi hayo mawili hasimu yalio na itikadi kali. IS inaendelea kudhibiti maeneo ya Mashariki ya Nangarhar na inalichukulia kundi la Taliban kama Adui.