Rais Samia Suluhu Hassan kesho anatarajiwa kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Kilimanjaro, ambapo pamoja na mambo mengine ataweka mawe ya msingi, kuzindua miradi ya maendeleo pamoja na kuzungumza na Wakazi wa mkoa huo.
 
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai amesema kuwa Rais Samia Suluhu Hassan atazindua barabara ya lami kutoka Sanya Juu – Elerai yenye urefu wa kilomita 32.
 
Kagaigai amesema, Rais pia ataweka jiwe la msingi katika ujenzi wa wodi ya Mama na Mtoto katika hospitali ya mkoa Mawenzi, na kisha ataweka jiwe la msingi katika ujenzi wa daraja la Rau pamoja na kuongea na Wananchi katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi.
 
Halkadhalika akiwa mkoani Kilimanjaro, Rais Samia Suluhu Hassan atashiriki Jubilee ya miaka 50 ya hospitali ya kanda ya KCMC.
 
Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwasili mkoani Kilimanjaro kesho jioni.