Rais Samia Suluhu Hassan, leo amewaapisha Viongozi mbalimbali aliowateua hivi karibuni.

Viongozi hao walioapishwa katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma ni pamoja na  Sofia Mjema aliyeapishwa kuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga na Jaji Omar Othman Makungu aliyeapishwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania.

Mwingine aliyeapishwa na Rais Samia Suluhu Hassan ni Jaji Mustapha Siyani ambaye ameapishwa kuwa Jaji Kiongozi.

Hafla hiyo imehudhuriwa na Viongozi mbalimbali akiwemo Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson na Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma.