Hukumu kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya imeanza kusomwa leo Ijumaa Oktoba 15, 2021 na Hakimu Mkazi Mwandamizi Odira Amworo.

Hakimu Amworo ameanza kusoma maelezo ya mashahidi 11. Kabla ya kuanza kusomwa hukumu, Wakili wa Serikali, Felix Kwetukia amesema Jamhuri ipo tayari kupokea hukumu.

Mawakili wa utetezi Moses Mahuna, Silvester Kahunduka na Fridolin Germelo pia wameeleza wapo tayari kusikiliza hukumu hiyo.

Hakimu Amworo amewaelekeza washtakiwa Lengai ole Sabaya, Silvester Nyegu na Daniel Mbura kukaa kusikiliza hukumu.