Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis ameyalaani mashambulizi ya hivi karibuni ya nchini Norway, Afghanistan na huko Uingereza ambako mbunge Davies Amess aliuawa kwa kushambuliwa na kisu. 

Papa Francis ametuma salamu za rambirambi kwa familia za wahanga huku akitoa mwito kwa watu kuachana kutumia njia ya kikatili ambazo mara zote husababisha hasara kwa pande zote, akitolea mfano mashambulizi hayo yaliyosababisha wengi kufariki dunia na kujeruhiwa. 

Aidha amesema wakati akitoa baraka za wiki hii jana kwenye kanisa la Mtakatifu Petro kwamba anawaombea jamaa wa wahanga wa mashambulizi hayo. 

Zaidi ya watu 140 walikufa katika shambulizi la kujitoa muhanga katika msikiti ulioko Kandahar nchini Afghanistan wakati nchini Norway kukishuhudiwa shambulizi la upinde na mshale lililosababisha vifo vya watu watano.