Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wamewasilisha taarifa ya kusudio la kukata rufaa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha leo Alhamisi Oktoba 21, 2021 ya kupinga hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha Oktoba 15.

Katika kesi hiyo Sabaya na wenzake watatu wamehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha.

Wakili Moses Mahuna amesema baada ya kuwasilisha taarifa ya kusudio hilo la rufaa taratibu nyingine zinaendelea.

Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Arusha, Odira Amworo baada ya kuridhika kuwa upande wa mashtaka umethibitisha mashtaka dhidi ya Sabaya na wenzake.