Mkosoaji wa serikali ya Urusi aliyefungwa jela Alexei Navalny amesema kwamba tume ya magereza imebadilisha hadhi yake gerezani na kumfanya mfungwa wa makosa ya ugaidi na itikadi kali. 

Hata hivyo haangaliwi kama mfungwa mwenye hatari ya kutoroka jela. Navalny amesema kupitia ukurasa wake wa Instagram kwamba amehojiwa mbele ya tume hiyo iliyopiga kura na kuamua kwa sauti moja kumbadilishia hadhi ya kifungo chake. 

Hatua hiyo inafungua nafasi ya kuzidi kuongezeka shinikizo rasmi dhidi ya mkosoaji huyo mkubwa wa rais Putin ambaye kwa sasa anatumikia kifungo cha miaka miwili na nusu jela kwa makosa ya kukiuka sheria ya kuachiwa kwa msamaha,makosa ambayo anasema yalitengenezwa kuzima malengo yake ya kisiasa.

Navalny amesema ameipokea hatua ya kutoonekana tena kama mfungwa mwenye hatari ya kukimbia na kwamba hatokaguliwa mara kwa mara usiku na walinzi. Kinachobadilika ni kwamba katika mlango wa chumba chake cha jela kutawekwa maandishi tu yanayoonesha ni gaidi.