Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetoa mkopo wa Tsh TZS 168.9 bilioni kwa wanafunzi 65,359 ambao majina yao yametangazwa katika batch 1, 2, 3 na 4 hadi sasa.
 
Kwa mujibu ya Bodi ya mikopo, Dirisha la Rufaa litafunguliwa Novemba 6, 2021 ili kuwapa fursa wanafunzi ambao hawajaridhika na viwango vya mikopo vya sasa kuwasilisha maombi ya kuongezewa.

Wakati tukisubiri bodi ya mikopo wafungue rasimi dirisha la kukata rufaa, tumeona ni vyema tukakuandalia makala inayoeleza kwa kina namna ya kukata Rufaa kwa wale watakaokosa mikopo au watakaopewa mkopo ambao kwa namna moja au nyingine wanadhani ni mdogo....
 
👉Tumekuandalia hatua 7 muhimu za kufuata wakati wa kukata rufaa.
 
KUMBUKA;
Awamu hii ya Rufaa huwa hakuna muda wa kuruhusu watu kufanya marekebisho baada ya ku-submit rufaa zao. Hivyo basi, kuwa makini mno kwenye kujaza data (taarifa) zako. Unaweza pia kumuomba mtu wako wa karibu akague ulichojaza ili kuona makosa unayoweza kuwa umeyafanya.
 
Vilevile, hakikisha attachments zote zinakuwa kwa mfumo wa PDF (Portable Document Format). Wakati ukiwa una-preview attachment husika hakikisha maneno yote yanasomeka vizuri, na mihuri yote inaonekana vizuri.
 
 
 
👉Kupata nafasi mbalimbali za kazi serikalini, mashirika binafsi <<BOFYA HAPA>>