Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani likiongozwa na Kamanda wa Polisi mkoa huo ACP Wankyo Nyigesa linamshikiliaAbdul Selemani miaka 27, Mluguru, Mfanyabiashara ya stationary mkazi wa Visiga kwa kipofu, Wilaya ya Kibaha Mkoa wa Pwani kwa kosa kutengeneza nyara za Serikali.
Kwamba Mnamo tarehe 12.10.2021 majira ya saa 11:38 jioni huko eneo la Visiga kwa Kipofu Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola walimkamata Abdul Selemani miaka 27, Mluguru, Mfanyabiashara ya stationary mkazi wa Visiga kwa kipofu kwa kosa la kutengeneza na kuuza vitambulisho vya Taifa vya NIDA na kuviuza Tsh 10,000/- kwa kila kitambulisho anachotengeneza.
Mtuhumiwa huyo amekamatwa na vifaa mbalimbali alivyokuwa anatumia kama vile;- Vitambulisho viwili vya Taifa vya NIDA, komputa mpakato, Pvc card, Desktop Computer, Monitor, Frash Disk na Printer.
Mtuhumiwa amekamatwa na atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.
KWA TUKIO LINGINE MTUHUMIWA ANAYEDAIWA KUTAPELI WATU MBALIMBALI AKAMATWA PWANI.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani ACP Wankyo Nyigesa amesema mnamo tarehe 14/10/2021 majira ya saa 10:00 jioni huko kwa mfipa, Wilaya ya Kibaha mkoa wa Pwani, Peter Baziro ambaye pia hutumia jina la Pius Jailos Nducha amekamtwa kwa kuwatapeli watu mbalimbali kwa kuwauzia viwanja na kughushi hati za viwanja anavyoviuza na hati za mauzo.Pia
Pia amekuwa akitapeli watu na kujipatia fedha kwa kuwauzia magari, mpaka anakamatwa amejipatia pesa kutoka kwa watu mbaliombali akiwemo Bi Jenifa Asa aliyemlipa mtuhumiwa kiasi cha Tsh (1,400,000/=) Milioni moja na laki nne kwa lengo la kumuuzia eneo la ukubwa wa 20 kwa 20 huku akijua kwamba sio kweli na hana eneo hilo.
Mtuhumiwa huyu amekuwa akibadilisha majina kila anapofanya tukio lakutapeli mtu ili asikamatwe. Baada ya mahojiano mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.
Jeshi la Polisi mkoa wa Pwani linaomba mtu yeyote aliyewahi kutapeliwa na mtu huyu afike kituo cha Polisi kibaha mji kwa utambuzi.