Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Afya Duniani WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus, ameyahimiza mataifa na makampuni yanayodhibiti ugavi wa chanjo cha ugonjwa Covid-19 kutoa kipaumbele kwa mpango wa kimataifa wa ugawanaji chanjo COVAX, ili kufikia malengo ya utoaji wa chanjo. 

Tedros amesema katika mkutano na waandishi habari kwamba wanashirikiana na viongozi kuunga mkono utoaji kipaumbele na upangaji unaohitajika kufanikisha lengo la kuchanja asilimia 40 ya wakaazi wa dunia, kwa kuchukuwa hatua kubwa na madhubuti.