Mkuu wa jeshi la polisi nchini, Simon Sirro, leo Oktoba 18, amezungumza kwa mara ya kwanza baada ya kukabidhi kijiti cha uenyekiti wa EAPCCO.. 

Amesema tangu Oktoba 14 hadi leo (jana) Oktoba 18, 2021 amekuwa katika mkutano  uliofanyika katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya (CONGO) kwa ajili ya kukabidhi  uenyekiti  wa Shirikisho la Wakuu wa Majeshi ya Polisi ukanda wa mashariki  EAPCCO ambao amehudumu kwa takribani miaka miwili baada ya kuongezewa mwaka mmoja kutokana na ugonjwa wa Corona(Covid-19).

Akikabidhi uenyekiti huo CPF Sirro amesema kuwa ameziambia nchi wanachama 14 juu  ya mafanikio yaliyopatikana kutokana na chuo cha Mafunzo ya wanamaji(Marine) kilichopo jijini Mwanza ambapo jitihada kubwa zimepatikana ikiwemo kuwakamata wahalifu na magari mbalimbali na kusaini mikataba na EAPCCO ambalo ni shirikisho la nchi nane ikiwemo Congo Brazavile, Guinea na Togo ambazo nchi hizo nazo zinaushirika wao ambao ni CAPCO ambazo zimesaini mkataba wa pamoja wa mashirikiano katika mambo makuu ya ulinzi sambamba na mafunzo ya pamoja, Upelelezi pamoja na oparesheni za pamoja kutokana na baadhi ya nchi hizo kuwa na matukio mbalimbali ya kihalifu kwa hiyo chuo  cha Marine Mwanza kitakuwa cha kimataifa katika masuala mazima ya mafunzo kwa CAPCO na EAPCCO.

Aidha CPF, Sirro ameeleza  kuwa hakuna changamoto lakini  kwa wanaojaribu kujihusisha na makosa ya ugaidi, usafirishaji haramu wa binadamu na madawa ya kulevya kutokana na ushirikiano huo wa nchi hizo wamekuwa wakiwakamata  na kuwafikisha watuhumiwa mahakamani kwa hiyo amewaomba watanzania kuendelea kuliamini Jeshi lao la Polisi kwani lipo imara kudhibiti uhalifu unaoweza kujitokeza.

"Naomba watanzania waelewe kuwa viashiria vya Uhalifu vinavyoweza kujitokeza mfano mauaji  uporaji kwenye mabenki na maeneo mengine hapa Tanzania hayapo tu hapa nchini kwetu,  bali yapo dunia nzima kwa hiyo cha msingi ni kutoa taarifa kwa vyombo vya dola ili kufanikisha kudhibiti uhalifu unaoweza kujitokeza"

"Polisi hatuwezi kumaliza vitendo vya kihalifu peke yetu pasipokuwa na ushirikishwaji wa wananchi kwa kutupatia taarifa, amani ni jambo muhimu katika mustakabali wa nchi, hata nyie waandishi wa habari hamuwezi kufanya kazi yenu vizuri kama hakuna amani, tuendelee kushirikiana katika kudumisha Amani" Alimalizia.